Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Sijali,
ARBEIT MACHT FREI, unafahamu maana yake? Maana yake ni LABOUR MAKES (you) FREE. Hayo ni maneno ambayo hadi leo hii yapo kwenye mageti ya kuingilia kwenye Concentration Camps ambako watu wengi sana waliuawa kwa kupigwa Risasi, njaa, magonjwa, maradhi na walipoona idadi ya kuuwa inaenda polepole sana, ndipo wakaja na Gas Chamber na baadaye kuchoma miili. Ila huwezi kuamini kuwa watu wa kwanza kabisa kuingia kwenye hizo Camps hawakuwa WaIsrael ila Wanasiasa wa Kigeruman kutoka chama cha kisocialist. Hiki ndicho kilikuwa chama kikubwa cha upinzani kwa Hitler na akaamuwa kuwamaliza kwanza hawa. Alivyowamaliza ndiyo akaanza kuhamia kwa Wayahudi, Wahungury, Wapolish, Rumunia na mataifa mengine mengi ambao walimpinga au kuwasaidia wayahudi.
Nafikiri tusibishane sana kwenye IDADI kwa sababu kwangu mie, haina maana sana. Kila roho ya binadamu inasimama yenyewe. Kwa hiyo auwe mmoja, wawili, mia moja au Milioni sita, haileti tofauti yoyote. Tuseme aliuwa watu laki tano (au nayo ni kubwa? Tuseme Elfu 50) ni watu wengi sana. La muhimu hapa ni kuwa ALIUWA na hii ni bila kujali kama alitumia GAS au risasi. Ila narudia tena, Wajeruman walipoona kuuwa watu kwa kutumia Risasi kunaenda polepole, ndipo walipokuja na Gas Chamber. Nafikiri nimekujibu hili kwa ufasaha.
Kila mtu anajua Netanyahu na Obama wanachukiana na nini lilikuwa chaguo la Wayahudi. Kuhusu Kennedy hakuna mwenye uhakika hadi leo ingawa ukweli ni kuwa FBI au CIA walihusika katika vifo vyote vya Kennedy Brothers na Martin Luther King.
Jimmy Carter walimmaliza Republicans kwa kutumia trick ndogo sana. Iran walikamata Askari wa USA na kuwaweka mateka. Carter alipeleka ndege kwenda kuwakomboa askari na eti ndege zikagongana. Ikazuka mzinga wa AIBU na Republican wakatumia hiyo sababu kuonyesha kuwa Rais Carter ni dhaifu. Hii ilifanyika karibu na uchaguzi na kweli uchaguzi ulipofika, Carter nje. Akaja Ronald Reagan na sakata zima la Iran likaishia wale askari kuletwa nyumbani bila kutumia maguvu na imekuja kujulikana kuwa Vigogo fulani wa Iran walitengeneza hela nzuri sana kwa kusaidia hilo zoezi la kubadilisha rais.
Nina uhakika kabisa kuwa ile film ya Mtume Mohhamed iliyopelekea kuchomwa kwa balozi za USA nchi za Kiislam na mwisho maofisa na balozi wa USA kupoteza maisha, ilikuwa imepikwa na Republicans. Romeney alijaribu kuitumia sana hiyo karata ila watu hawakuinunua. Alianza hata kudai Obama hakutangaza mapema kuwa ni Magaidi wamefanya hivyo. Ilifika hatua, Obama kwenye Debate akampa za usoni Romeney kuwa "Gavana, usisahau kuwa mie ni "Chief in Commader" na jamaa akanywea. Watu walipogoma kumpinga Obama kwa mashambulizi ya Waislaam wenye Siasa kale, nikaona na Bibi Netanyahu kanywea.
Angalia hizi film hapa uone uhusiano wa Obama na Netanyahu:
https://www.youtube.com/watch?v=GnSVsE_xYxk
https://www.youtube.com/watch?v=zJ9UzCm_eDk
https://www.youtube.com/watch?v=iuQvgLeyvgs
https://www.youtube.com/watch?v=6kEnDcNojFg

Last edited by a moderator: