pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 19,030
- 15,232
Hivi jamani huyu mtu ni timamu kweli kichwani kwake? Huu upuuzi alikuwa anaongea na nani? haya majisifu wanayaweza 'wanawake tu.
We mzima kweli umesikia utumbo anaongea Bashite au unakurupuka kama uharo?Nyinyi bula kumtaja Paul Makonda mnahisi hamjafanya siasa kwa siku hiyo.
Bavichaa mnayo matatizo
Ana wowowo la kuvutia.Nyinyi bula kumtaja Paul Makonda mnahisi hamjafanya siasa kwa siku hiyo.
Bavichaa mnayo matatizo
Instagram inaharibu akili za watu.....mkuu jitahidi kuwa unaujua ukweli utaishi vizuri sana.Salaam, baada ya salamu nauliza, Unamtetea Makonda kwa hoja ipi?
Raisi wetu ana msemo wake anaoupenda sana kwamba MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU, Nami nasema kwambaa ukweli ni kuwa MAKONDA HANA SIFA YA KUWA KWENYE NAFASI ALIYOPO. Haijalishi utapima kwa vigezo gani lakini mwisho wa siku ukweli utabaki kuwa hivyo, Hastahili kuwa kwenye nafasi aliyopo.
Pamoja na kwamba sikumpigia Raisi wetu kura yangu, lakini mimi nilikuwa miongoni mwa Watanzania wengi sana ambao miezi kadhaa ya mwanzo wa uongozi wake tuliona tumaini kwa taifa letu, tumaini la kwamba walau tumempata kiongozi ambae ana nia ya dhati ya kuirudisha nchi yetu katika muelekeo sahihi, Kwangu mimi kilichonipa tumaini kilikuwa pale nilipomuona Raisi bila woga na hofu alipoamua kulivalia njuga suala la vyeti feki. Mimi naamini ili hii nchi iendelee ni lazima tuwe na mfumo imara wa elimu yetu, mfumo ambao mwanafunzi akimuona engineer kwenye TV usiku huo akeshe akiwa darasani akisoma kwa kujua kuwa njia pekee ya kufika pale ni kusoma kwa bidii.
Hata alipowaita wale vijana wa UDOM Vilaza nilimtetea raisi wangu maana nilijua alikuwa anafanya kitu sahihi kusafisha mfumo wa elimu yetu ili mtu aliyesoma aheshimike kwa elimu yake. Nimesikitika sana kuona kwa sababu ya mtu mmoja tu, raisi amelirudisha taifa kule kule lililokuwa na kuondoa kabisa matumaini ya mabadiliko kwa Tanzania yetu hii.
Kama kiongozi wa Uma, Makonda alitakiwa mara tu zilipotoka na kuanza kusambaa taarifa za yeye kufoji vyeti alitakiwa mara moja atoke hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hilo, hivyo ndivyo viongozi wa uma wanatakiwa kufanya, Tuliona Mh Mwigulu alifanya, Juzi kuna kiongozi pale Kenya katoa pia vyeti vyake kwa tetesi tu za yeye kufoji vyeti, Kwanini Makonda yeye ananyamaza?
Kunyamaza tu kwa kiongozi wakati kukiwa na tuhuma kama hizo tayari imemuondolea uhalali way eye kuwa kiongozi katika nafasi yake. Hata kama ni kweli ana uwezo wa kufanya kazi, hana tena credibility ya kuongoza wananchi ambao asilimia kubwa wanamuona kama mdanganyifu, na zaidi sana wanamuona kama Kilaza. Nafasi aliyopo haitakiwi kuwa na kiongozi ambae wananchi wana mashaka nae.
Anasimama anasema yeye kuwa pale ni Mpango wa Mungu? Hilo linamaanisha nini? Kwaiyo tuwaambie watoto wetu wasihangaike kusoma badala yake wasali sana ili siku moja Mungu awaweke kwenye nafasi kama yake? Kufeli si dhambi, lakini ni kosa kubwa sana kudanganya. Nilishangaa sana kuona raisi analifumbia macho hilo pasipo kufikiria athari zake kwa taifa letu. Je wewe unamtetea Kwa hoja ipi hasa?
Mwisho, Raisi wangu umetukosea sana Watanzania tulio wengi kwa sababu walau tulishaanza kuwa na matumaini na wewe, lakini kwa sababu ya personal affection kwa mtu mmoja umeamua kuzipuuza sauti za wananchi wako na kuamua kumtetea mtuhumiwa, Umetukosea.
ukweli upi?Instagram inaharibu akili za watu.....mkuu jitahidi kuwa unaujua ukweli utaishi vizuri sana.
Inaonekana umetokea kolomijeInstagram inaharibu akili za watu.....mkuu jitahidi kuwa unaujua ukweli utaishi vizuri sana.
Na wewe nenda kampikie mumeo huko acha ubashiteNyinyi bila kumtaja Paul Makonda mnahisi hamjafanya siasa kwa siku hiyo.
Bavichaa mnayo matatizo
Bangiii mbayaInstagram inaharibu akili za watu.....mkuu jitahidi kuwa unaujua ukweli utaishi vizuri sana.