Video: Mwananchi akamatwa baada ya kuidai serikali huduma ya maji

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,669
Katika hali isiyokua ya kawaida mwananchi wa sengerema amejikuta mikononi mwa polisi kwa kitendo chake cha kuidai serikali huduma ya maji,hii imetokea baada ya kuwataja viongozi wa serikali hasa Rais wa Tanzania katika suala zima la kudai maji.

NB# Namshukuru Mungu sina rafiki wala ndugu polisi kwa sasa.
 
Katika hali isiyokua ya kawaida mwananchi wa sengerema amejikuta mikononi mwa polisi kwa kitendo chake cha kuidai serikali huduma ya maji,hii imetokea baada ya kuwataja viongozi wa serikali hasa Rais wa Tanzania katika suala zima la kudai maji.

NB# Namshukuru Mungu sina rafiki wala ndugu polisi kwa sasa.View attachment 2947918
Kwanza nianze kumshukuru Rais Mama Samia kwa kukamatwa wanao dai maji!
 
Katika hali isiyokua ya kawaida mwananchi wa sengerema amejikuta mikononi mwa polisi kwa kitendo chake cha kuidai serikali huduma ya maji,hii imetokea baada ya kuwataja viongozi wa serikali hasa Rais wa Tanzania katika suala zima la kudai maji.

NB# Namshukuru Mungu sina rafiki wala ndugu polisi kwa sasa.View attachment 2947918
Hizi video za police stupidity actions zinasambaa sana duniani na kuiweka nchi yetu kwenye mstari wa nchi kandamizi jambo ambalo ni kweli...

Unadai maji. Polisi anailinda serikali isikuletee maji. anakukamata na unafunguliwa faili la kuisumbua serikali kwa kuidai huduma ya maji.

Samia, anapoyaona haya na kuyanyamazia ni dalili ya wazi anaunga mkono huu ukatili wa polisi
 
D
Katika hali isiyokua ya kawaida mwananchi wa sengerema amejikuta mikononi mwa polisi kwa kitendo chake cha kuidai serikali huduma ya maji,hii imetokea baada ya kuwataja viongozi wa serikali hasa Rais wa Tanzania katika suala zima la kudai maji.

NB# Namshukuru Mungu sina rafiki wala ndugu polisi kwa sasa.View attachment 2947918
Dah hii nchi bana anachodai na kuongea ana haki nayo kikatiba , lakini mamlaka wametumia nguvu huenda kosa lake ni dogo kuliko haki aliyoiongea

Huenda kosa lake ni namna ya ufikishaji ujumbe. Lakini angefikisha je siku hizi ili ujumbe uwafikie walengwa ambao huwafikii kirahisi lazima ujitoe ufahamu.

Mkimpiga mmemuonea na kuvunja sheria na kumkamata mmekosea sheria yeye hajavunja sheria huenda amekiuka maadili ya ufikishaji.
 
Tunampongeza Raisi Samia na jeshi la police kwa kufanikisha kukamatwa kwa mwananchi huyu anataka huduma ya maji safi..
Na nitoe rai kwa raiya kuacha kudai maji safi mana kipaumbele cha mama ni Treni na ndege asantee
 
Hapana ni ya mwezi huu wa 3 niliona kwenye taarifa ya habari ITV, mara ishafika huku Jukwaani!!
 
Back
Top Bottom