Mungu wangu, hii yoote kuwatisha watu wasiende kwenye mikutano ya wapinzani, ikiwezekana CCM iendelee kuwa madarakani, kwani wakiondolewa, siri zoote zitakuwa wazi kwa mfano:-
1. Kifo cha Sokoine hakitakuwa fumbo tena.
2. Kifo cha Holace kolimba wahusika watafahamika na wananchi watajua ni nani aliyewatuma wafanye mauaji yale.
3. Kifo cha Imrani Kombe kitaangaliwa upya, na kutakuwa na fursa ya kohoji kwanini wauaji waliachiwa huru na kwa maslahi ya nani
4. Ufisadi wa melemeta utahojiwa, kupata ukweli kama kweli ulikuwa ni mradi wa Usalama wa Taifa na kama kweli Usalama wa Taifa wanafanya biashara.
5. Kutakuwa na fursa ya kuwabana wale wezi wa Pesa za EPA ambao walisamehewa na Kikwete na kuwaomba warudishe ilihali, kuna watu wamebainika kuiba Baiskeli wanaozea jera.
6. Kutakuwa na fursa ya kujua kama kweli Pesa ya EPA imerudishwa yoote au ilikuwa ni funika Kombe Chadema ipite.
7. Kutakuwa na fursa za kuhoji uhusika wa Kikwete katika ishu ya Richmond, japo Lowassa alitaka kutudokeza lakini alisita.
.
.
.
.
.
.
.
.
6548. Kutakuwa na fursa ya kujua kuna siri gani ya kuendelea na watu kama akina Kamuhanda japo ametajwa katika mauaji ya Songea na Iringa?
6549. Itafahamika kama Balali alifariki kweli au yupo hai, na kama yupo hai kwanini afichwe?