VIDEO - Mauaji Ya Kutisha Norway, Awaua Watu 84 Kwa Kuwapiga Risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Mauaji Ya Kutisha Norway, Awaua Watu 84 Kwa Kuwapiga Risasi

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jul 28, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  <tbody>[TR]
  [TD="colspan: 3"]VIDEO - Mauaji Ya Kutisha Norway, Awaua Watu 84 Kwa Kuwapiga Risasi[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD] [​IMG]
  Baadhi ya wahanga wa shambulio la risasi kwenye kisiwa cha Utoya nchini Norway[/TD]
  [TD] Saturday, July 23, 2011 8:38 PM
  Norway imekumbwa na simanzi kubwa baada ya mwanaume mwenye msimamo mkali wa kikristo mwenye kufuata siasa za mrengo wa kulia akiwa amevaa unifomu za polisi aliwaua zaidi ya watu 84 kwa kuwapiga risasi.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"] Mwanaume mwenye umri wa miaka 32 raia wa Norway ambaye ameelezewa kuwa ni mkiristo mwenye siasa kali ambaye alikuwa akitumia tovuti za kikristo kutuma meseji za kuupinga uislamu na wahamiaji nchini Norway, anashikiliwa na polisi kwa mauaji ya zaidi ya watu 92.

  Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Anders Behring Breivik anatuhumiwa kufanya shambulio kubwa la bomu alilolificha kwenye gari lililopaki karibu na jengo la ofisi ya waziri mkuu wa Norway, Jens Stoltenberg.

  Watu saba walifariki dunia kutokana na shambulio hilo kubwa ambalo liliutikisa mji mkuu wa Norway, Oslo.

  Baada ya kufanya shambulio hilo, Anders alipanda kivuko na kwenda kwenye kisiwa kidogo cha Utoya ambako mkutano wa vijana zaidi ya 500 wa chama tawala ulikuwa ukifanyika.

  Dakika 90 baada ya shambulio la kwanza, Anders akiwa amevaa nguo za polisi aliwakusanya vijana hao akidai amekuja kuwasaidia lakini badala yake alianza kuwamiminia risasi akisema "Lazima nyote nyie mfariki".

  Kwakuwa shambulio hilo lilitokea kwenye kisiwa, baadhi ya watu walikimbilia baharini kunusuru maisha yao, lakini Anders aliendelea kuwamiminia risasi huko huko kwenye maji.

  Maji yenye baridi kali ya baharini yaliwafanya baadhi ya watu washindwe kuogelea na kurudi kwenye kisiwa hicho ambapo muuaji huyo aliendelea kumimina risasi.

  Waliokimbilia kwenye msitu aliwafuata huko huko na kuwamiminia risasi.

  Jumla ya watu 84 wamethibitishwa kufariki kwenye shambulio kwenye kisiwa hicho ingawa idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka wakati polisi wakiendelea kusaka maiti baharini kwakuwa baadhi ya watu inaaminika walizama maji wakati wakiogolea kunusuru maisha yao.

  Anders amefunguliwa mashtaka kwa mashambulio hayo mawili ambayo yamepelekea jumla ya vifo vya zaidi ya watu 92.

  Angalia VIDEO za mashambulio hayo chini.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]
  VIDEO - Mauaji Ya Kutisha Norway


  VIDEO -Simanzi Yatanda Norway


  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kijana mtaalam huyo
  kwa imani yake ataiona pepo!!
  RIP
   
 3. KAKA A TAIFA

  KAKA A TAIFA JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Imani ni itikadi na ni ugonjwa ukiingia akilini ni ulevi
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,001
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Mashujaa kama hao wanahitajika sana TZ,tena angefaa kukaa pale magogoni tungekuwa hatuna vijisenti wala wakina jeuri,nchi inge nyoooka.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
Loading...