VIDEO: Maisha ya Rais Kikwete baada ya kustaafu asema maisha ni mazuri sana

paulivo

Member
Jan 22, 2016
15
2
Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Akizungumza na mwandishi wa BBC Tulanana Bohela kuhusu shughuli anazozifanya kwasasa

kikwete.jpg

Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete aliondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka kumi. Je, wajua anafanya nini siku hizi?
Msikie Rais Mstaafu hapa kwenye hii video
 
Sema safari za ndege zimepungua sio kama alipokuwa kazini, aseme ukweli tu jamani kwi kwi kwi kwi
 
Kwa wastaafu wengine waliolitumikia taifa hili kwa zaidi au karibia miaka 30 wakistaafu maisha yao ni taabu tupu maana siku anayostaafu mshahara unasimama siku hiyo hiyo,ambapo Mifuko ya hifadhi ya jamii haiwalipi mapema mafao yao inachukua hata zaidi ya miezi sita ndiyo inawalipa licha ya kwamba walikuwa wanakatwa kutoka kwenye mishahara yao midogo kuchangia akiba ya uzeeni hali kadhalika mwajiri alikuwa anamchangia asilimia fulani kwenye akiba ya uzeeni ya mtumishi husika,ni ajabu mtumishi akistaafu anaambiwa mfuko hauna fedha hakika maisha ya mstaafu ni tabu tupu
 
NI VIZURI KUJIPANGA KABLA ASEE
 
NI VIZURI KUJIPANGA KABLA ASEE
Kweli kujipanga nivizuri. Lakini pia moja ya mipango baada ya kustaafu ni jinsi ya kutumia hayo malipo ya mifuko ya hifadhi unayoyapata, sasa yakichelewa maisha ya kustaafu hanakuwa magumu kwa kiasi fulani.
 
huyu toz kaharibu sana nchi hii japo yapo mema yke ....!

lkn sometimes nkimsikiliza najikuta naenjoy( nacheka sana ) hasa ktk kuchukulia mambo easy easy na vidharau kmtindo...! haaaah
 
Nikimwona huyu baba nakumbuka tulivyodanganywa"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"
 
Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Akizungumza na mwandishi wa BBC Tulanana Bohela kuhusu shughuli anazozifanya kwasasa

kikwete.jpg

Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete aliondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka kumi. Je, wajua anafanya nini siku hizi?
Msikie Rais Mstaafu hapa kwenye hii video

Huyu mtu ni feki sana, anastahili akamatwe na ahukumiwe kwani aliuza nchi kinyemela.
 
Binadamu bwana! MTU aliwahi kuwa Mbunge, kabla ya ubunge aliwahishika nyadhifa ndani ya chama, akawa waziri, baadae rais wa nchi kwa miongo 10, bado ni mwenyekiti wa chama, ni mjumbe wa aman nchini Libya, ni makamo mwenyekiti wa tume ya afya ya mama Na mtoto kimataifa, sasa hali yake itakuwaje mbaya? Acheni chuki jamani hamuwezi kumfikia kawaacha mbali sana
 
Back
Top Bottom