Hiyo kitu imesha wahi tokea kifanya nadhani miaka kama 10 iliyopita pembezoni mwa mlima kifanya.... Volcano eruption
Nimeishi kifanya mwaka mzima ndo nasikia leo kwenye hui uzi.ni uongo uliotukuka
Kifanya haijawahi tokea kitu kama hicho
Miaka kumi iliyopita mlima Kifanya ulitoa lava lakini haikuwa na nguvu ya kuja kutokea kileleni kwa hiyo ilitawanyika bondeni huko ambako wakazi wanalima bustani za maharage maarufu kama vinyungu,ninachokumbuka ni kwamba ulikuwa tu kitu kama udongo mweupe sanaaaa uliochanganyikana na chembe nyeupe nilikuwa darasa la saba kipindi hicho,baadae nilikuja kusoma kuwa ni "quartz" madini yanayotumika kutengenezea machemli ya taa za mafuta,kwahiyo hakukuwa na moto wala lava hiyo haikuwa ya moto ilikuwa ni cold lava.
Nisimulie sasa baadhi ya maajabu ya mlima Kifanya na maeneo ya jirani na mambo yake za ajabu.
Zamani juu ya mlima huu kulikuwako na kijimsitu kidogo sana ingawa kipo mpka Leo ila kimeshaharibiwa kidogo,kulikuwako na kuku wengi weupe waliokuwa wakiishi huko bila kufugwa na mtu yeyote,ilikuwa unaruhusiwa kuenda huko na ukitaka ukamkamata na kumla huko juu ni Sawa ila sharti usishuke nao kabisa,nakumbuka kila ikifika msimu wa mavuno wakulima walioondoka Kifanya kwenda kulima Dodoma walikuwa wanarudi kufanya matambiko huko juu na sharti kuwa kuku wa kutumiwa ni wa hukohuko mlimani,hili nimeshuhudia kwa macho yangu ingawa kwa sasa hakuna Tena Hayo mambo baada ya makampuni ya Simu Kujenga minara kwa Hayo watu wengi wanafika na eneo kubwa kukaribia kileleni kumepandwa miti ya mbao.
Nilifanya ziara kule nikiwa la saba ila majibu mengi nimekuja kupata baada ya kuwa sekondari na chuo.
Maana kuhusu lava kulikuwa na imani potofu nyingi sana kumbe ilikuwa ni kitu rahisi sana.
Ziko stori nyingine kuhusu sehemu inayoitwa "matundu ga simba"
Kuhusu mzungu aliyefika kulima viazi liwengi na kupotea ghafla baada ya kupata Mali iliyoachwa na babu zake zamani,aliacha kila kitu kuanzia Matrekta,greda na miundombinu yoootee.Story nzuri sana hii kwa wanaoijua.
Kuna Habari kuhusu kuwako kwa madini ya uranium eneo la mpocho ambako mambo ya ajabu hutokea eneo hilo.
Story kuhusu igaba,ngo'ongwa na lyaso.
Zote ninazo.
Hiyo ya kisima sijawahi sikia,labda imetokea miezi ya karibuni hivi baada ya Mimi kuja kutafuta riziki mikoa ya watu