Mr. Policeman, tunakudis kitaani, kama Ferouz alivyoimba kweli hawana cha kufanya zaidi ya kubambikia kesi wananchi. Kuna Binamu yangu yeye kasomea mambo ya electronics na ni fundi TV wakati huo, siku moja alipigiwa simu na jamaa anayemfahamu aende akachukue TV kwake imeharibika, kama saa 12 jioni hivi jamaa akaenda akaicheki akagundua ina hitilafu kwa hiyo inahitaji kwenda workshop ikafanyiwe kazi, akatoka pale alipo kaibeba kichwani na fundi mwenzie si mbali na home kwake mwendo kama wa dk tano tu hivi, njiani akakutana na Polisi wawili, wakamhoji unapeleka wapi TV usiku huu, jamaa akajitetea kuwa yeye ni fundi na anaipeleka ile TV workshop, polisi wakadai nyie ndo wezi wenyewe leta risiti ya kununulia TV, jamaa akasema kama vipi twendeni kwa mwenye TV mkadai hiyo risiti polisi hawakuhitaji maelelzo zaid wakamkamata na kwenda naye polisi post wakamweka 2days pale mpaka habari zilipotufikia jamaa tayari alikuwa keshabambikiwa kesi ya kuua ya mtu aliifanya songea huko na ilibaki siku moja tu angepandishwa kizimbani, ilibidi kutoa kilo nzima kuifuta ile kesi hiyo ilikuwa ni miaka ya 2000-2001. Jeshi hili limeoza SANA TUUU, hakuna anayesema ukweli huko