VIDEO: Je Kikwete aliwaendesha ovyo Diaspora kuja kuwekeza Tanzania au tatizo liko kwa Magufuli?

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,380
5,871
Ndugu zangu naomba mnipe ufafanuzi wa hizi siasa za Tz na watanzania waishio nje,Raisi K aliwaomba watanzaia waje Tz kujenga nk,alinifuahisha zaidi alipotoa mfano hai wa nchi ya Israel ilivyojengwa na waiziraili waishio nje ya Israeli...

Watanzania wanaoishi nje ya wengi waliwekeza wakati wa Kikwete sasa wanataka
kunyanga´anywa walichowekeza....je hii ni haki, je Tanzania hakuna siasa ya kuaminika,je ni chuki,je ni visasi, je........?

Sikiliza vizuri maneno ya Kikwete halafu toa mawazo yako

Tusaidiane kimawazo,,,

Ndugu zangu naomba mnipe ufafanuzi wa hizi siasa za Tz na watanzania waishio nje,Raisi K aliwaomba watanzaia waje Tz kujenga nk,alinifuahisha zaidi alipotoa mfano hai wa nchi ya Israel ilivyojengwa na waiziraili waishio nje ya Israeli...

Watanzania wanaoishi nje ya wengi waliwekeza wakati wa Kikwete sasa wanataka
kunyanga´anywa walichowekeza....je hii ni haki, je Tanzania hakuna siasa ya kuaminika,je ni chuki,je ni visasi, je........?

Sikiliza vizuri maneno ya Kikwete halafu toa mawazo yako nini haya.

Tusaidiane kimawazo,,,

jamani kwani kuwa diaspora ni cheo? Au utumwa? Raia aliyepo nje ya nchi na Raia aliyepo nchini wote wana haki sawa hakuna aliye bora kuliko mwingine
 
Mwenye uraia wa nje lazima awekeze kwa kutumia company. ..mbona halijaaribika jambo lolote?
 
Mwenye uraia wa nje lazima awekeze kwa kutumia company. ..mbona halijaaribika jambo lolote?

Mkuu umeisikiliza hiyo video vizuri,umemsikia nini Dr K aliwambia hao watu, au ndio yale yale huyu anasema hivi yule anasema vile,sheria inasema hivi

Serikali kama serikali lazima iwe na msimamo hasa kwa jambo kama hili,katika hiyo video Dk K kasema "watu lazima waje kujenga nyumba Tz .....bla bla bla"
 
Unajenga kwa kutumia jina la company yako. ...mbona ndugu zangu wengi sana wanamiliki nyumba kwa njia hiyo? Nenda wizara ya ardhi watakufafanulia vizuri sheria inasemaje. ...Anyway good luck
 
Unajenga kwa kutumia jina la company yako. ...mbona ndugu zangu wengi sana wanamiliki nyumba kwa njia hiyo? Nenda wizara ya ardhi watakufafanulia vizuri sheria inasemaje. ...Anyway good luck

Sheria inasema hivyo,lakini hivyo sivyo Kikwete,alivyowambia watu wa Diaspora,halafu usifikiri kila mtu anaeishi ulaya au nje ya Tz anauwezo wa kufungua Company,nafikri kwa mawazo yangu mafupi, kama raia wa nje unataka kuvungua kampunini Tz lazima uwe na mtaji wa kiasi fulani cha pesa ili lamupuni yako isajiliwe.....,sio kila mtanzania na 100,000 dollars za kuwekeza TZ...,,

Hao ndugu zako wako vizuri,wengine wanaosha vyoo wanapeleka pesa kidogo kidogo nyumbani kusaidi wazee na jamaa uwezo huo hawana,tafakari
 
huyu waziri ni kilazah anaturudisha miaka mingi nyuma ,Kikwete alishatoa mwelekeo na alikuwa ndie anayewahimiza warudi kuwekeza nyumbani ...leo huyu anaharibu kabisa ......mabenk ,na taaisi nyingine zilizowekeza kwa diaspora zifanyeje .....Iitabidi yule kijana KAINERUGABA MSEMAKWELI akaendeleze ile kesi yake ......no wounder huyu aliyekuwa mwalimu wa chipukizi standard seven leaver ambaye hajawahi kujiendeleza leo naye ana degree ya political science .......
kwanini magufuli anaonea watumishi wenye vyeti feki vya la saba anawaacha hawa ......mimi naona aliyenunua jina standard seven akalitendea haki hadi akawa daktari kama Kigwangwala huwezi kamwe kumlinganisha na aliyeishia la saba alafu akanunua degree..
wote tunajuwa miaka ya nyuma kufaulu la saba ilikuwa ishu walikuwa wanaita kuchaguliwa ....kuna mikoa haata upate wastani mzuri huwezi kuchaguliwa kwa ajili ya ushindani kwa hiyo walikuwa wanahamia mikoa mingine kurudia
Na kuna mikoa ambayo kutokana na mwamko duni mtu anachaguliwa lakini hataki kwenda hapo utamlaumu vipi mtu kama Hamis kigwangwala kwa kulitendea haki jina la kijana aliyepata bahati akakataaa shule ....
 
Back
Top Bottom