Video ikimuonesha bosi wa Hamas Ismael Haniyeh alipopokea kwa mara ya kwanza taarifa ya vifo vya vijana wake na vijukuu

The Stress Challengerr

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
2,479
6,764
Video hapo chini ikimuonesha kiongozi mkuu wa kundi la Palestina Hamas Ismail Haniyeh
akipokea kwa mara ya kwanza taarifa za vifo za vijana wake watatu Hazem, Mohammed na Amir pamoja na wajukuu zake wanne Mona, Amal, Khaled and Razan.

Sauti inasikika ikitoa ujumbe kwa Haniyeh ambaye alikuwa ziarani hospital Qatar kuwatembelea wapalestina waliojeruhiwa vijana wako watatu na wajukuu zako wanne wameuwawa.

Haniyeh akaonekana kidogo na mshtuko alipopata habari na kujikaza na kubaki mkakamavu kabla ya taratib kutembea kutoka kwenye chumba na Kusema Allah azilaze roho zao mahali pema.

Akaulizwa na msaidizi wake kama wanaweza kukatisha ziara hiyo ya kutembelea wagonjwa? Haniyeh kwa ukakamavu akajibu hapana na kwa nini wakatishe akasema waendelee.

Baadaye alitoa kauli kupitia Aljazeera kwa kumshukuru Allah kwa kumpa heshima kupitia vifo vya vijana wake na vijukuu.

Kiongozi huyo mkuu wa Hamas aliendelea kusema madogo wangu wametunukiwa hii heshima. Walibaki na watu wetu wapalestina Gaza, hawakuondoka na kukimbia. Damu za madogo wangu siyo za thamani sana kuliko damu za watu wetu.

Ismail Haniyeh aliendelea kuiponda Israel eti inaendeshwa na roho ya kisasi akidai ameshapoteza ndugu na wanafamilia 60 tangu hii vita ianze.

The terror leader hit out at Israel, stating they are 'driven by the spirit of revenge' as he claimed around 60 members of his family have been killed since the start of the war.

Hao viongozi wa Hamas wangeomba UN iwakutanishe na viongozi wa Israel wamalize tofauti zao na kukubaliana tuweke silaha chini tuishi kwa amani tuunde serikali moja tushirikiane na tuheshimiana kwa dini zetu bila kuchukuana. Je amani haiwezi kupatikana?
 
Ila huyu kiongozi wa Hamas ni jasiri. Kipimo cha mwanaume ni kifua na anapopokea habari za kifo cha wapendwa wake.

Kwenye Biblia mfalme Daudi dogo wake aliyezaa na Bethsheba (Bethsheva kiibrania) mrembo aliyemuiba kutoka kwa Huriah alipokuwa anaumwa alilia sana na kufunga na kumuomba Mungu asimuue. Lakini Sir godi alivyomtwaa mwamba Daudi akachangamka piga msosi wa nguvu kuoga paka marashi na kuendelea na majukumu yake ya ufalme royal engagements hadi wafanyakazi na wasaidizi wake wakabaki kushangaa WTF! Yani dogo kafa badala Daudi ahuzunike yeye ndo kwanza kachangamka nakuendelea na maisha kama hamna msiba
Aisee
 
Kupoteza Watoto 3 kwa mpigo na Wajukuu 3 ni Jambo gumu sana lakini msijifanye hamnazo mnajua kabisa Israel ndio mvamizi katika maisha kuna muda unafika unabakia na option 2 kufa au kuwa mtumwa.Haneya kachukua ya kwanza wanae wamekufa.Sote tutakufa ila usife kitandani kwa mke wa mtu ufie nchi yako ndio akili.
nyie Tz mnaibiwa sana mnajifanya uoga hakuna uoga wa heshima kunguru muoga anaheshimika?? Eagle ni Jasiri ana heshimika.

Netenyahu nae siku zake zikifika atakufa
 
Video hapo chini ikimuonesha kiongozi mkuu wa kundi la Palestina Hamas Ismail Haniyeh
akipokea kwa mara ya kwanza taarifa za vifo za vijana wake watatu Hazem, Mohammed na Amir pamoja na wajukuu zake wanne Mona, Amal, Khaled and Razan.

Sauti inasikika ikitoa ujumbe kwa Haniyeh ambaye alikuwa ziarani hospital Qatar kuwatembelea wapalestina waliojeruhiwa vijana wako watatu na wajukuu zako wanne wameuwawa.

Haniyeh akaonekana kidogo na mshtuko alipopata habari na kujikaza na kubaki mkakamavu kabla ya taratib kutembea kutoka kwenye chumba na Kusema Allah azilaze roho zao mahali pema.

Akaulizwa na msaidizi wake kama wanaweza kumaliza ziara hiyo ya kutembelea wagonjwa? Haniyeh kwa ukakamavu akajibu hapana na kwa nini wamalize akasema waendelee.

Baadaye alitoa kauli kupitia Aljazeera kwa kumshukuru Allah kwa kumpa heshima kupitia vifo vya vijana wake na vijukuu.

Kiongozi huyo mkuu wa Hamas aliendelea kusema madogo wangu wametunukiwa hii heshima. Walibaki na watu wetu wapalestina Gaza, hawakuondoka na kukimbia. Damu za madogo wangu siyo za thamani sana kuliko damu za watu wetu.

Ismail Haniyeh aliendelea kuiponda Israel eti inaendeshwa na roho ya kisasi akidai ameshapoteza ndugu na wanafamilia 60 tangu hii vita ianze.

The terror leader hit out at Israel, stating they are 'driven by the spirit of revenge' as he claimed around 60 members of his family have been killed since the start of the war.

View attachment 2960968
Angeanza kulia ningeshangaa,hawa jamaa kuhusu kifo kwao ni kwaida kabisa.

Ndio maana kuua mtu kwao ni sawa na kuchinja kuku tu.
 
Hao viongozi wa Hamas wangeomba UN iwakutanishe na viongozi wa Israel wamalize tofauti zao na kukubaliana tuweke silaha chini tuishi kwa amani tuunde serikali moja tushirikiane na tuheshimiana kwa dini zetu bila kuchukuana. Je amani haiwezi kupatikana?
Wewe unadhani vita hivyo ni vya kidini ?
 
Haya maigizo ni kawaida sana kwenye hizi video, wekeni video za siri bila maandalizi yoyote muone uhalsia, mzee kizazi chake kimefutwa baada ya yeye kuchinja watoto wa Wayahudi.
Hamna kitu kibaya kama mzee kwenye umri huu unazika watoto na wajukuu wako badala ya wao wakuzike wewe. Unaondoka duniani bila faida yoyote kwa jamii.
Siku nyingine mpunguze shobo kwa Wayahudi, endeleeni kuchinja Wakristo lakini temaneni na Wayahudi.
Waburuza dera akina brazaj mjifunze sana
 
Hao viongozi wa Hamas wangeomba UN iwakutanishe na viongozi wa Israel wamalize tofauti zao na kukubaliana tuweke silaha chini tuishi kwa amani tuunde serikali moja tushirikiane na tuheshimiana kwa dini zetu bila kuchukuana. Je amani haiwezi kupatikana?
Watu tunajadili hii ishu ya Palestina na Isarael kwenye dini lakini tatzo lao ni ardhi kila mtu anaamini pale ni asili yao. Hii vita haitakwisha kwa kuwa tunaendelea kuzaana.
 
Back
Top Bottom