KWELI Video hii imetengenezwa kwa akili unde

KWELI Video hii imetengenezwa kwa akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Huku ukieleza nyenzo ya kidigitali uliyotumia, bainisha picha halisi iliyotumika kutengeneza video hii.

1764488515040.png
 
Tunachokijua
Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la maudhui yanayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde yanayosambazwa mtandaoni hasa picha na video ambayo yamekuwa yakipotosha uhalisia.

Mfano picha halisi inaweza kutumika kutengeneza video isiyo halisi kwa kutumia Akili Unde jambo linaloweza kusababisha upotoshaji unaweza kuibua tharuki na kusababisha madhara kwa jamii.

Rejea video iliyohifadhiwa hapa ilichapishwa katika mtandao wa TikTok ikionesha tukio lisilo la kawaida ambapo inaonekana ndege kubwa inayopaa usawa karibia na watu pamoja na majengo huku vitu vilivyopo chini vikionekana kupata msukosuko wa upepo uliotokana na ndege hiyo.


Uhalisia

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika viashiria vinavyoonesha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia Akili Unde.

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia sehemu ya picha ya video hiyo (Screenshot) kwa kutumia Google Reverse image search umebaini picha halisi ilichapishwa katika tovuti mbalimbali kutoka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuanzia mwaka 2020 na kueleza kuwa ni eneo la Bunia, Ituri nchini humo. Rejea hapa, hapa, hapa na hapa.

Vilevile video hiyo ina mapungufu yanayokinzana na uhalisia jambo linalodhihirisha kuwa imetengenezwa kwa aakili unde. Mathalani baadhi ya watu kuungana miili, kubadilika kwa mavazi ya watu, baadhi ya watu kupotea, gari kubebwa na upepo huku mwamvuli ukibaki kuwa imara jambo lisilo la kawaida.​
Kwa kutumia nyenzo ya yandex pamoja na google reserve image search inabainisha kuwa picha halisi imepigwa katika eneo la kituo cha kamanda wilaya ya ituri nchini Congo.
kwa mjibu wa tovuti ya la kivupost inabainisha kuwa picha hii ilipigwa mara baada ya ajali mbaya ambayo ilitokea siku ya jumatano july, 3.2024
picha halisi iliyotumika kutengeneza video hii ni
ORIGINAL PICTURE.jpg
 
Kwa kutumia nyenzo ya yandex pamoja na google reserve image search inabainisha kuwa picha halisi imepigwa katika eneo la kituo cha kamanda wilaya ya ituri nchini Congo.
kwa mjibu wa tovuti ya la kivupost inabainisha kuwa picha hii ilipigwa mara baada ya ajali mbaya ambayo ilitokea siku ya jumatano july, 3.2024
picha halisi iliyotumika kutengeneza video hii ni
Haya sema upewe Nini mkuu
 
Ila AI inatikwa ifundishwe zaidi, kwenye video gari inetupwa mbali na upepo wa ndege, lakini binadamu aaah wapo tu na mambo yao
 
Back
Top Bottom