Video: Haj Manara awashukia Waislamu

Video: Haj Manara awashukia Waislamu

Kwa hiyo wewe unamzidi manara kujua uislamu?!
Mwenzako alishakusa mkufunzi wa dini
Hahahaa! Kwahiyo unaona manara kichwa sana kwenye dini, huyo manara alimpa Nandy 50mil ili amwimbie twiga wake ambae sasahivi kakimbia, hiyo 50m angeipeleka madras mwalimu angekuwa na maisha gani?
 
Hahahaa! Kwahiyo unaona manara kichwa sana kwenye dini, huyo manara alimpa Nandy 50mil ili amwimbie twiga wake ambae sasahivi kakimbia, hiyo 50m angeipeleka madras mwalimu angekuwa na maisha gani?
Ww unaamini kabisa manara na milion 50 yakumpa nandy ili amuimbe demu wake?!
 
Pengine Sio Tone nzuri ya kubembeleza lakini kwa jambo hili naamini nilikuwa sahihi!

Haiwezekani tusifiane Wafanyabiashara wengi ni Waislaam kisha Maimamu wengi wanaotuswalishia Miskiti yetu na Waalimu wanaotufundishia Watoto wetu elimu ya dini wawe omba omba na malofa!!

Tufikirie sasa kutengeneza mifumo sahihi itakayoondoa kabisa hili tatizo kwa jamii yetu!!

Mtu akiwa Imaam au Ustaadh wa Madrasa licha ya kulipwa malipo mema na Allah lakini tuwalipe vizuri ili kazi wanayoifanya iwe na thamani duniani na akhera Insha'Allah 🙏🙏

Nb: Msisahau tukifa hawa tunaowadharau hv sasa ndio wanaotustiri kwa kutuosha na kutuweka Makaburini


Hutba nzima ya shehe Haji Manara


View: https://m.youtube.com/watch?v=f_xe29BwYzw
 
Sadaka zinatakiwa za kuendeshea misikti sio kulipwa hao mashekhe,
Mashekhe wakatafute kazi za kufanya uzuri kwenye uislamu yoyote anaruhusiwa kuendesha swala hataa kama ni mtoto mdogo ukifika muda wa ibaada hakuna aliye wekwa alama lazima awepo yeye ndio mambo yaende kama upande wa pili..
Isipokuwa swala za jamaa.
Ndugu Midekoo Kama nilivosema awali mimi nipo upande wa kukazia tu
mimi naendelea kukazia mkuu waumini waongeze nguvu kutoa sadaka. i know what am saying (hisani ya mkoloni)

mimi nipo upande wa kukazia tu


Suala la waumini kuongeza nguvu kwenye sadaka nililikazia kwa sababu rasilimali fedha na mali ni muhimu sana kuendesha baadhinya mambo kwa uhuru na nafasi.

Kama ukipata muda naomba upitie mjadala ha huyu jamaa aliouanzisha siku kadhaa hapa nyuma tweets za kwanza nimeshindws kuambatanisha ila tutumie hii alokuja kama kuhitimisha baada ya kupata backlash ya hapa na pale baina ya waumini wengine wakiunga mkono wengine wakipinga.

Nachoomba mimi upitie comments za hiyo tweet pamoja na quote tweet zake. Naamini utakubaliana nami kwamba waumini waongeze bidii ya sadaka


View: https://x.com/Addy_Adams/status/1914206167980548191

Naweka nakala moja kwa Malaria 2
 
Back
Top Bottom