Kwa dar kama unataka ku test Aura ama mkuki mall unazipata wanachezesha.
Kwa kununua mwenyewe.
1. Best setup utahitaji
-VR headset toka Oculus ama HTC itaku cost angalau laki 5 kuendelea
-machine inayoweza kusukuma Games za VR angalau gtx 1060 itahitajika, desktop waweza tumia tu hizi za mtaani i5 4th gen minimum, hapa around 2m itahitajika.
-gimmick yoyote kama Gari, bubduki ama kitu chengine ambacho kitaongeza ladha.
Hivyo at minimum angalau milioni 3 inaweza kuzidi.
2. Setup ya kawaida
Hapa unaweza nunua Oculus Go ama VR nyengine ambayo ni standalone, hizi ni as cheap as $150 kwenye sale, hivyo around laki 4 Unapata, hutahitaji chengine chochote, Sema hutapata content za pc utapata vigame uchwara na content kidogo. Ila kwa ushamba wetu zinafaa kibiashara.
3. Setup ya kimasikini.
Nunua headset kwenye MITUMBA hadi 5000, Tafuta na simu yenye kioo cha QHD amoled kama s6, s7, note 5 etc hata refurb zile zinafaa, chomeka simu kwenye headset enjoy vr, njia hii ndio kabisa haina content, ukishindwa kabisa njia za juu iwe last resort.