VIDEO - Familia Ambayo Watoto Wa Kiume Wanaota Matiti Kama Wanawake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
6450126.jpg

Mmoja wa watoto wa familia ya Ramirez ambayo watoto wa kiume wamekuwa wakiota matiti kama wanawake

Saturday, June 02, 2012 8:39 PM
Inakuwaje pale watoto wa kiume wanapoota matiti makubwa kama vile ni wanawake?, hali kama hiyo imeitokea familia moja katika jamhuri ya Dominica ambapo watoto wote watatu wa familia hiyo wana matiti makubwa kama ya wanawake hali inayowafedhehesha kutokana na jamii kuwachukulia kama vile ni mashoga.
Watoto wote watatu wa kiume katika familia ya bwana Felipe Ramirez, walikuwa wakizomewa na kuchukuliwa kama mashoga na baadhi ya watu sababu kubwa ikiwa ni kutokana na matiti makubwa kama ya wanawake waliyo nayo.


Watoto hao ambapo mkubwa ana umri wa miaka 17 na mdogo wa mwisho akiwa na umri wa miaka 11, wamekuwa wakipata tabu katika maisha yao ya shule na nyumbani kutokana na jamii kuwachukulia tofauti.


Yeuri mwenye umri wa miaka 17 na mdogo wake Gabriel mwenye umri wa miaka 11 pamoja na Daniu mwenye umri wa miaka 12, wamekuwa wakiishi na baba yao baada ya mama yao kuwakimbia watoto hao wakiwa na umri mdogo.


Baba yao hakuwa na uwezo wa kuwapeleka hospitali kupatiwa matibabu ya kuyaondoa matiti hayo hali iliyowafanya waendelee kuishi maisha ya fedheha kwa miaka yote hiyo.


Kilio cha baba yao kwenye vyombo vya habari kuomba msaada kilisikika mwezi huu baada ya hospitali ya arcelino Velez Santana Hospital kuamua kuwafanyia operesheni ya kuondoa matiti hayo ambapo gharama za operesheni zitalipwa na bosi wa hospitali hiyo Dr Pedro Antonio Delgado.


Watoto hao wamefanyiwa operesheni ya kuondoa matiti hayo na hatimaye hivi sasa wanaweza kutoka mitaani bila ya kutupiwa maneno ya kejeli na watu.


Madaktari wamesema kuwa wataendelea kuyafuatilia maisha ya watoto hao na watawapa dawa za kuzuia kuendelea kuzalishwa kwa homoni za kike zilizokuwa zikisababisha kukua kwa matiti hayo.


Angalia VIDEO chini kujionea maisha ya mwanzo ya watoto hao na maisha yao ya sasa baada ya kufanyiwa operesheni ya kuyaondoa matiti yao.




VIDEO - Familia Ambayo Watoto Wa Kiume Wanaota Matiti Kama Wanawake








[video]http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=645012 6&&Cat=7[/video]
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom