Tatizo lake iingine anajifanya anaijuwa Kenya kuliko mtu yeyote. Anasahau kuwa na yeye wenzie wanamjua kuliko anavyowajuwa. Ana misimamo ya ajabu lakini misomamo haitamsaidia kitu, akubali tu ushirikiano na wapinzani ili nchi isonge mbele
Muhimu akubali kushirikiana na wapinzani. Haiingii akilini watu wanapata asilimia 45%-48% za kura wote unawaweka benchi. Hapo kunaweza kuwa na margin of error. Labda wenyewe ndio washindi. Busara ingetumika.
Husikilizi wala kuwapa nafasi serikalini. huu mfumo umepitwa na wakati. Africa inabidi wadau wote washirikishwe kwenye maamuzi, mipango na utekelezaji wa serikali. Tunahitaji mfumo mwingine.
Kenya pia walikosea kuifunga nchi wakati wa COVID, nchi ilikuwa imefungwa miaka miwili baada ya hapo, kampeni, uchaguzi, maandamano. Pia walichukua mikopo mingi ya COVID ambayo ilienda kwa viongozi wachache.
Kwahiyo shughuli nyingi za uzalishaji za kiuchumi zilisimama.