Video: Dr. Slaa ndani ya Washington D.C., USA

Video: Dr. Slaa ndani ya Washington D.C., USA

ZeMarcopolo,
Mawazo yako ni ya kipuuzi. Josephine ni mke wangu. Hata mkisema namna gani hakuna atakayebadilisha kwa kuwa ndoa ni kati ya watu wawili. Mungu tu ndiye atakayehukumu kwa kuwa ndiye anayejua nafsi na mioyonya wanaoingia kwenye Mkataba. Mnapoteza muda kuzungumzia ndoa ya Slaa na Josephine, wakati jamii ya watanzania wanamkubali na wamempokea Josephine Kama Mke wa Dr Slaa. Ni watu Kama wewe na CCM waliofanya kila jitihada kwenye magazeti na hata kusukuma watu kwenda mahakamani. Hayo yote hayabadilishi status ya Slaa na Josephine.

Pili, swala la Josephine kuingilia masuala ya Chadema, tafadhali kwa manufaa ya wasomaji wa JF na wanachadema kwa ujumla weka hadharani ni masuala gani ameingilia, na ni kifungu gani cha Katiba kimevunjwa. Kwa wengi msiofahamu, Josephine ni mwanaharakati tangu kabla hatujafahamiana. Matunda ya kazi zake yanaonekana kwenye mitaa ya Keko, Kinondoni, na Kimaria. Dr Slaa ni mwana demokrasia, na Siko tayari kuzuia vipaji na wito wa mtu. Shughuli hizo zinategemea moyo wa mtu na Mungu wake, ndio maana si kila mtu anaweza kufanya kazi hizo. Kama ambavyo ninawashawishi, ninawasukuma, ninawajenga uwezo watanzania mbalimbali kuwahudunia watanzania wenzao, kuwashirikisha watanzania katika ujumla wao katika kazi ya ukombozi wa Taifa letu. Kila mmoja wetu ni sawa na pingili ya Chain, na wote tunahitajiana. Asiyepingana na sisi yuko na sisi, alimradi kila mmoja wetu anatumia karama alizopewa na Mwenyezi Mungu. Wote tukiwa wanyenyekevu na kutambua Hilo kazi ya ukombozi itakuwa nyepesi.

Swala la Josephine kutumia ID ya Dr Slaa, is a none Issue. Rudi kwenye post ya Josephine. Alieleza kuwa Hana access ya Internet kwenye IPAD yake. Alikuwa mnyofu kuwa julisha wasomaji na japo ID ni ya Dr Slaa, akasaini Kama Josephine. Sasa hapo issue nini? Kama kuna agenda nyuma ya hapo si itamkwe wazi badala ya kuzunguka zunguka. Ni kukosa uadilifu kutunga mambo ya kipuuzi dhidi ya mtu mwingine. Ustaarabu nimkuwa Kama mtu hakuelewa alikuwa na haki ya kuuliza lakini siyo kuhukumu, navkueneza propaganda. Katika dini zetu umbea, majungu na kudanganya au kupotosha ni dhambi. Kama kweli kuna nia njema ni muhimu kuwa wakweli na wawazi katika yote tunayofanya. Ukweli na uwazi hutufanya kuwa na uhuru wa kweli vinginevyo mtaendelea kuishi katika unafiki na utumwa wa nafsi zenu wenyewe. Nimetumia lugha kali kwa kuwa hoja za kipuuzi zinapoteza muda bila sababu, muda ukipotea kwa umbeya na majungu tunapoteza fursa za kujenga Taifa letu ambalo kila Leo linazidi kutumbukia kwenye umaskini na kero mbalimbali. Tunahitaji kuweka nguvu pamoja, bila kujali itikadi kupambana na kero ili tujenge Taifa letu. Hakuna atakayejenga Tanzania isipokuwa Watanzania,lakini watanzania watakaojenga Taifa Lao siyo haw a ambao kila kukicha wanazungumza watu, tena kwa kuchanganya uwongo na propaganda. Kama kila anayechangia angetumia sehemu ndogo sana ya ubongo wake constructively, Tanzania ndani ya muda mfupi sana itajikomboa. Amerika iliendelea kiuchumi, kimaendeleo kwa kuwa hawana muda na majungu, umbeya wala upuuzi tunaosoma kila Leo kwenye Mitandao na hasa JF. Kila mmoja anatumia muda alionao kujiendeleza na kuendeleza Taifa lake. Mitaani hutaona ushabiki na propaganda za vyama, ndio hakuna ushabiki wa kushindania bender za vyama, badala karibu kila nyumba inapepea bendera ya Taifa Lao America. Watu wako proud na Taifa Lao na union wazi kwa jinsi wanavyosifia kila kitu cha kwao. Tujifunze hatujachelewa, tubadilike vinginevyo watoto na wajukuu watatulaani kwa kutokuwajengea mazingira mazuri Kama Mungu alivyokusudia.

Omba radhi kwa dharau uliyowafanyia wafuasi wako wachache...
 
slaa ni janga la kitaifa

Nikusaidie kuwa kama taifa ni ufisadi na wizi wa mali za watanzania na kufanya wachache kula keki ya taifa na mamilioni ya watu wakikosa huduma muhimu basi hapo ni sawa kuwa Slaa ni janga la taifa la namna hiyo. Kwa maneno mengine Slaa ni janga kwa CCM a.K.a Taifa kama ulivyosema
 
Omba radhi kwa dharau uliyowafanyia wafuasi wako wachache...

Ameongea point tupu sema tu kwa vile Wabongo akili zetu tumezibinafsisha sijui wapi tutaendelea kumkejeli.Dr Slaa analipenda Taifa lake kuliko nyinyi mnavyodhani.Nani alijua kama Nchi ilikuwa inatafunwa mabilioni kwa mabilioni ya shilingi na mafisadi,Baadhi ya WanaCCM walijua lakini kwasababu ya uwoga wao na kukosa kwao uzalendo hawakuthubutu kufunua midomo yao kuzungumzia huu ufisadi wa kutisha na mikataba mibovu vilivyofanywa na Serikali lakini kwa UJASIRI,UZALENDO,MAPENZI kwa Nchi yake Dr Slaa akisaidiana na Kijana wake Zitto Kabwe waliamua kujitoa mhanga kwaajili ya Watanzania wengine ili kuwafumbua macho kuhusiana na uchafu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya Watendaji na Vigogo wa Serikali dhidi ya fedha za Walipa kodi wa Tanzania pamoja na rasilimali za asili za Nchi hii.Ila kama ilivyo kawaida ya Watanzania na tatizo lao sugu la kumbukumbu mshasahau mazuri yote ya Dr Slaa sasa mnamuona adui wenu namba moja.
 
Back
Top Bottom