Linus w slaa
Member
- Jan 29, 2025
- 67
- 151
CCM Nzasa Watishia Kukatwa Mgombea Wao Hawatashiriki Uchaguzi
Chama cha Mapinduzi (CCM) Nzasa wametoa salamu kali, wakisema kuwa iwapo mgombea wao atakatwa na kwa sababu zozote, hawatashiriki uchaguzi wa Oktoba 2025. Kauli hii inakuja wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani, ambao tayari umeanza kuwa na mvutano wa kisiasa.
Wakati huo huo, chama cha upinzani cha Chadema kimeendelea na kampeni yao ya "No Reforms, No Elections," wakisisitiza kuwa hawashiriki uchaguzi bila mabadiliko ya kina katika katiba na sheria za uchaguzi. Chadema wamesema wazi kuwa bila tume ya uchaguzi huru na uhuru wa kisiasa, kushiriki uchaguzi kungekuwa ni kuhalalisha mfumo wenye kasoro. Kauli hii imepata umaarufu mkubwa mtandaoni na katika maongezi ya kitaifa, ingawa CCM wamejaribu kuiponda.
Hata hivyo, CCM Nzasa wamechukua msimamo wa kipekee kwa kuwatishia kuwa wanaweza kutoshiriki uchaguzi kabisa iwapo mgombea wao ata katwa, jambo ambalo linaweza kuongeza mvutano zaidi katika siasa za Tanzania. Wataalamu wa siasa wanasema msimamo huu unaweza kuwa ni jibu la shinikizo la Chadema, lakini pia unaonyesha woga ndani ya CCM kuhusu mustakabali wa uchaguzi.