VIDEO - Ajichoma Moto Kupigania Uhuru, Afariki Dunia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
6333482.jpg

Jamphel Yeshi akikimbia mbele ya watu huku akiwa amejichoma moto, alifariki dunia baadae

Wanaume wawili toka nchini Tibet wamejichoma moto kuupinga utawala wa China kwenye nchi hiyo, mmoja wao amefariki dunia baada ya kuungua asilimia 98 ya mwili wake.
Jamphel Yeshi kijana mwenye umri wa miaka 27, alijichoma moto nchini India kupinga ziara ya rais wa China nchini India na kuuonyesha upinzani wa raia Tibet ambao wamekuwa wakipigania uhuru wao toka China.

Jamphel ambaye alikuwa akiishi nchini India baada ya kuondoka Tibet miaka mitano iliyopita, alijichoma moto na kukimbia umbali wa mita 50 mbele ya kadamnasi ya watu waliojitokeza kupinga ziara ya rais wa China nchini India.

Jamphel alidondoka chini baada ya kuzidiwa na moto huo, jitihada za kuokoa maisha yake hazikuzaa matunda, Jamphel alifariki dunia alipofikishwa hospitali.

Mwanaume mwingine naye alijichoma moto kwenye tukio kama hilo lakini yeye alinusurika maisha yake.

Zaidi ya watu 30 raia wa Tibet walijichoma moto wenyewe mwaka jana katika kuonyesha upinzani wao kwa serikali ya China ambayo imekuwa ikiitawala Tibet kwa zaidi ya miaka 50.

Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.

<span id="lblFull" style="display: inline-block; width: 469px; ">


VIDEO - Ajichoma Moto Kupigania Uhuru, Afariki Dunia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom