Victoria Group wamefia wapi?!

Super Handsome

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
3,844
Reaction score
6,470
Bandugu,

Wakati wa utawala uliopita kuliibuka kundi maarufu lililo sheheni watu wa kada mbali mbali hasa kutoka kanda ya ziwa lililoitwa "Victoria Group"

Kundi hili lilihusisha Wafanyabiashara, wanasiasa, wanataaluma mbalimbali, matapeli wapigaji na watoto wa mjini, wanamuziki na vibopa mbali mbali wa makampuni binafsi na serikali nk.

Pamoja na mambo yote kundi hilo pia lilikua linatajwa kua na matumizi makubwa sana ya anasa!

Moja ya mikakati yao ilikua ni "Kumpachika" MTU mmoja (Mwanachama mwenzao) kushika moja ya nafasi za juu kabisa za uongozi nchini!

Rais aliyepita analifahamu vizuri sana hili kundi!

Hata aliyewahi kua Mwanasheria wa "Voda" baadaye akaja kuukwaa uwaziri wa "Dhahabu na Almasi" alikua mwanachama kindaki ndaki!

Hili kundi lipo? Ajenda yao ilifanikiwa kwa kiasi gani? Kwanini Mara baada ya "MTU kutoka kwetu" kushika hatamu halisikiki? Vikao vyao vinafanyika wapi sikuhizi?

Kwa wale watoto wa mjini kama Pasco wa JF watakua na taarifa zao tu.. Hebu tupeane updates mwenye taarifa vigogo na ma-Pdg hawa ?
 
Bado wanaendeleza kula bata kwa mtindo wa kumchinja mbuzi au nguruwe mdogo mdogo kisha anatolewa utumbo woote anajazwa pilau kisha ana okwa..baada ya hapo ni mwendo wa Bapa na masanga mpaka kukuchee?? Tujuzane
 
kundi limepotea baada ya lengo lao kutotimia, na wengi wao walikuwa wapiga dili, sasa vyuma vimekazwa sana hawana pa kupumulia
 
mzee kipara lengo lake lilikuwa ni kushika usukani, sasa alipopata udereva, akaona itatakiwa alipe fadhila, ndio hapo sasa, kawachinjia baharini wenzake
 
wapo kibao waliokuwa wana lia lia, kuna yule jamaa mmiliki vya vyombo, mwingne wa majarida, wote hao walikuwepo
 
wapo kibao waliokuwa wana lia lia, kuna yule jamaa mmiliki vya vyombo, mwingne wa majarida, wote hao walikuwepo
Na wengi kati yao walikua na hardtops, ford rangers n Prado..kwahiyo unataka kuniambia hata yule Ngosha wa "vyombo" alikua ana mchngo mkubwa? Kwanini "Mwanasheria" wa Voda aka Mzee wa Kwalalumpa hakupenya na alikua na ushawishi mkubwa kundini?
 
nionyeshe paku subscribe mkuu
Click uzi wenyewe, halafu ukiona kama umekuwa na kijivuli hivi, nenda upande wa kulia pembeni juu kina vidoti vitatu vya ... Ila vimesimama wima, ukibonyeza yatakuja maandishi tofauti, wewe chagua Subscribe. Au Follow....
Kama unatumia simu lakini
 
Click uzi wenyewe, halafu ukiona kama umekuwa na kijivuli hivi, nenda upande wa kulia pembeni juu kina vidoti vitatu vya ... Ila vimesimama wima, ukibonyeza yatakuja maandishi tofauti, wewe chagua Subscribe. Au Follow....
Kama unatumia simu lakini
natumia pc mkuu
 
Click uzi wenyewe, halafu ukiona kama umekuwa na kijivuli hivi, nenda upande wa kulia pembeni juu kina vidoti vitatu vya ... Ila vimesimama wima, ukibonyeza yatakuja maandishi tofauti, wewe chagua Subscribe. Au Follow....
Kama unatumia simu lakini
Vile vile njia rahisi ni hapo hapo juu utaona alama ya Tick √ ukiigusa tu tayari ume subscribe
 
natumia pc mkuu
Kwa PC kama unatumia App ya Jf yenyewe bila kupitia OperaMini au Browsers nyingine. Process ni hizo hizo... Ila kwa PC kuna nyepesi hiyo ya Alama ya vema! Ukibonyeza tu, utaona inakuambia ume subscribe tayari.
 
Victoria group bado ipo, sema kuna mambo hayatakiwi kuwekwa hadharani kwa kipindi hiki lakini baada ya utawala wa Magufuli kupita kundi hili litakuwa na nguvu kubwa kuliko hapo awali.
Kwanini liwe na nguvu baada ya' na si wakati huu?

Nikijenga dhana kwamba madhumuni ya uwepo wa kundi hilo ni kumyumbisha kiobgozi ambaye si "wa kwao" nitakua nakosea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…