Vichekesho vya baadhi ya Wabunge wa CCM Bungeni

Vichekesho vya baadhi ya Wabunge wa CCM Bungeni

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
12189056_10156118276010198_5966610985503106529_n.jpg



Mheshimiwa Spika, kabla sijaingia kuchangia bajeti hii, nataka niseme kuwa naona

upinzani wamefikia pabaya sana, wanaikashifu serikali sikivu ya CCM.


Chama kimefanya mengi sana,

maendeleo makubwa tumepata,

shule za msingi, sekondari na vyuo viko vingi sana

tofauti na zamani,


barabara za lami, umeme nchi nzima mpaka vijijini, lakini wapinzani wanakebehi.

Naipongeza sana serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, bila kupoteza muda sasa niingie kwenye jimbo langu, naomba nielezee

kwa kifupi

matatizo ya jimbo langu.


Kule hatuna shule za sekondari katika kata sita, maji ni ndoto, tunategemea mvua za

msimu. Shule zilizopo hazina ubora wala walimu wa kutosha.


Rais alikuja sasa ni miaka sita akatuahidi umeme lakini mpaka

leo hakuna lolote.


Barabara ni mbovu hazipitiki.

Nauliza ni lini serikali hii ITATUSIKIA NA KUTULETEA

MAENDELEO?? (Wabunge Makofi)

kwa! Kwa! Kwa!.


Naombeni sana tena sana jimbo langu liangaliwe kwa jicho la

Huruma.


Baada ya kusema hayo

Mheshimiwa Spika, naunga mkono bajeti kwa 100%

Vipi wewe Mbunge wako anawateteaje Bungeni?

chanzo.http://jewajua.com/vichekesho-vya-baadhi-ya-wabunge-wa-ccm-bungeni/3471


 

Attachments

  • Vichekesho vya baadhi ya Wabunge wa CCM Bungeni.jpg
    Vichekesho vya baadhi ya Wabunge wa CCM Bungeni.jpg
    101.9 KB · Views: 1,286
Hahah! Aksante mkuu Mzizi Mkavu. We will miss mama speaker
 
Hahahahaha ccm ni ileile nawabunge ni welewale eeee niwalewale.
 
Masoud Kipanya ana akili pana sana,ukiitafakari cartoon #07 utapata maana kubwa sana,huko tuendako kama bunge halikupata usimamizi mzuri tatayaona haya.
 
Back
Top Bottom