Vichaa wawili walipanga mkakati wa kutoroka kutoka hospitali ya vichaa Mirembe.
Mpango wao ulikuwa kwamba asubuhi ya siku inayofuata waende getini wamvamie mlinzi wampige wafungue geti watoroke.
Kesho yake asubuhi wakaamka mapema kama walivyopanga wakaelekea getini lakini kwa bahati mlinzi hakuwepo na geti lilikuwa liko wazi. Vichaa hao wakasikitika sana na kuambizana.
Haaaa, mpango wetu umeharibika mlinzi hayupo twende tutajaribu siku nyingine.