Vicent Nyerere: CCM kichaka cha wahuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vicent Nyerere: CCM kichaka cha wahuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 26, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kampeni za uchaguzi wa ugombea udiwani zimezidi kuwasha moto wakati tukielekea siku ya uchaguzi ambayo ni tarehe 28/10/2012 siku ya Jumapili.Halikadhalika kampeni hizo zimeendelea mkoani Shinyanga hususani kata ya Mwawaza ambayo ushindani mkubwa upo kati ya CCM na CDM.

  Leo kwenye viunga vya uwanja wa shule ya msingi Ugimbagu,mh.Vicent Josephat Nyerere amewatahadharisha wananchi wa kata hiyo kuwa makini wanapofanya maamuzi mazito juu ya mstakabali wa maisha yao kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kumchagua kiongozi atayeweza kutekeleza shida na matakwa ya wana Mwawaza.

  Huku akimnadi mgombea wa chama chake cha CDM,mh Vicent amewashangaa wananchi ambao miaka zaidi ya hamsini hawana huduma muhimu za kijamii kama vile maji,umeme na huduma za afya lakini wanathubutu kuing'ang'ania CCM,wakati CCM ina wenyewe.

  Imekuwa ni desturi kwa CCM kuwakumbuka wananchi wa kata hiyo kila inapofika kipindi cha uchaguzi huku ikinadi ahadi mpya kabisa na kusahau kuwa wameshindwa kutekeleza ahadi walizo ahidi huku siku za nyuma.Akiwasihi wananchi hao ambao kwao huduma ya maji inaonekana kama anasa alisema CM ya leo si CCM ya mwalimu J K Nyerere,CCM ya mwalimu iliwajali wananchi na ilikuwa kweli CCM ya wakulima na wafanyakazi lakini leo hii CCM imekuwa kichaka cha wahalifu mbalimbali ambao wanatumia pesa chafu kuhakikisha wanapita katika chaguzi mbalimbali ili waweze kusimamia maslahi yao binafsi.

  Uchaguzi wa ndani ya CCM umethibitsha kuwa mlalahoi hana nafasi ndani ya chama tofauti na CCM ya mwalimu.CCM ya mwalimu ni sawa na CDM ya leo ambayo inawajali wananchi wake na kuwapigani kwa hali na mali kufanikisha maisha yao na rasilimali zao zinasimamiwa kwa manufaa ya umma.

  Akibeza tabia iliyojitokeza leo ndani ya chama tawala,ameshangazwa na kauli ya M/Kiti kukiri utitiri wa rushwa ndani ya chaguzi za chama huku akishindwa kuzifuta chaguzi zote ambazo zimekichafua chama.

  Akilaani matukio ya uvunjivu wa amani ndani ya kata hiyo, yeye kama waziri kivuli wa mambo ya ndani amemtaka waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha watu wote waliofanya tukio la kushambulia M/kiti wa tawi la Mwawaza kwa kumchoma mkuki kukamatwa mara moja ikiwa na kuwatia nguvuni wale wote walio washawishi vijana hao kufanya ukatili kama huo vinginevyo ajiuzuru nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani.

  Tukio hilo la kushambuliwa M/Kiti huyo limeibua simanzi kubwa miongoni mwa wananchi wa kata hiyo na kukosa kabisa imani na serikali ya CCM. Nikiongea na mmoja wa wakazi wa maeneo ya Ugimbagu, mwananchi huyo amelaani kitendo alichofanyiwa kiongozi wao na kusema, matokeo ya serikali kuwatelekeza wananchi kwa zaidi ya miaka hamsini malipo yake ni kuwapiga mishale na risasi za moto.
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good vicent, hit them hard
   
 3. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo dogo ni nooma, waulizeni watu wa arumeru mashariki.amesema kweli ccm ni kichaka cha wahuni kama majambazi,waganga wa kienyeji nk.
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  CCM- kina wenyewe, asili yao Msoga
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Real hard, with iron fist.
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Vicent Nyerere ni hazina kubwa sana ndani ya CHADEMA anajua kujenga hoja kama huamini omba umkute jukwaani....
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka mpambano wake na Ben Mkapa..Mkapa ilibidi akimbilie kwa Maria Nyerere kuomba suruhu...
   
 8. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mgombea nafasi ya udiwani kupitia CHADEMA Mh. Anthony Peter alipopata nafasi ya kuomba kura aliwashukuru wanachama wa CDM kwa kumuamini na kumuombea kipidni chote alipkuwa hospitalini akitibiwa jeraha lake la risasi na kubambikiwa kesi ya ujambazi kitendo kilichokuja kuthibitishwa na mahakama hana hatia.

  Aliwataka wananchi wamchague yeye kutokana na vipaumbele vyake vya maendeleo kwa watu wa Mwawaza,akipigania kupata huduma ya maji ,umeme na huduma ya afya ambayo wameikosa kwa zaidi ya miaka hamsini toka Tanzania kupata uhuru.Huku akibeza ahadi za mpinzani wake toka CCM za kuwajengea machinjio ya kisasi na uwanja wa ndege kwaajili ya kusafirishia nyanya ilihali uwezo wa wananchi hao ni duni na eneo lote la Mwawaza haliana hata bucha la nyama.Akiponda ahadi hizo aliitaka CCM kupitia mgombea wao kuacha tabia ya kuwahada wananchi kwa ahadi kubwa wakati haziendani na mahitaji halisia ya sehemu husika.
   
 9. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Yani mistari hiyo hapo juu ni tafsiri sahihi ya ccm ya sasa wala hamna haja ya kuongeza maneno mengine kupata tafsiri ya hiyo ccm.

  Hongera Vicent kwa ufafanuzi fasaha na sahihi wenye lugha nyepesi, fuatilia minyukano ya wagombea katika chaguzi za ndani za ccm ndio utajua kinachoendelea ndani ya ccm.

  Hawana sera tena za kuwafanya wachaguliwe na wananchi tukawapongeza. Angalia vituko ndani ya uwt. Mwenyekiti yupo na ameona na kusikia lakini cha ajabu huyo mama simba anapeta tu tena anakaa meza kuu na mwenyekiti huku wafuasi wao wakipiga makofi na kuimba kama MAZUZU vile.
   
 10. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukombozi wa fikra chanya ndani ya Taifa letu ni kila mmoja kuwa mchunga wa mwenziwe wakati wa mchakato wa chaguzi mbalimbali kuhakikisha hakuna anaye thubutu kuuza haki yake ya kupiga kura kwa kuuza kipalata chake cha kupigia kura,ikiwa pamoja na kuwakata na kuwazomea kila wapitapo kama ilivyofanyika kule Arumeru Mashariki kwa dogo janja
   
Loading...