BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,009
- Thread starter
- #21
Halina uhusiano wowote kwa sababu Lema si Mtanzania. Inaposemwa "Justice for all" ni kwa Watanzania tu. Hata baadhi ndani ya CCM wameanza kusema hadharani tena bila woga wa kumung'unya. Mwinyi, "Nchi inaenda kama gari bovu haina sukani" Warioba, "Nchi imepoteza muelekeo" Butiku, "Rais anayejiona yeye ni Tembo hatufai Watanzania. Hawa si wapinzani hawa ni watu ambao wamewahi kushika nafasi za juu Serikalini katika awamu mbali mbali lakini hawaridhishwi na muelekeo wa nchi. Pamoja na wao kuwa wanachama wa muda mrefu tangu enzi za TANU hadi CCM lakini wameona umuhimu wa kujitokeza hadharani na kuonyesha kutoridhishwa na hali hali ya nchi. Hata hawa bila shaka watakuwa ni wapiga majungu wazuri sana wafanya ujinga na wamejaa porojo tu ambazo hazina msingi wowote ule.
Wacheni Majungu, swala la Lema lina uhusiano gani na aliyosema VP? Hakuna hata moja mwenye ushahidi kwamba Lema anashikiliwa bila kufuata taratibu na sheria za nchi. Mwenye ushahidi kama anao ana nafasi ya kuifungulia kesi Serikali ya Tanzania mahakama kuu. Huu ulimbukeni wa kutoa maneno ambayo hamuwezi kufanya ni ujinga, tuache porojo, hivi nyinyi kweli mngeweza kusimamia haki wakati Tanganyika ilipokuwa inagawanywa na wazungu? Au mngeweza kupigania haki kama kina Mkwawa et al. Hizi porojo fanyeni majumbani kwenu mmeuziwa mbuzi kwenye gunia mmekaa kimya mtaweza kweli kuongoza nchi kweli au mnaangalia pua zenu tu.