Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,630
- 11,096
Habari, wana-JF naomba kueleweshwa kuhusu vibali vinavyohitajika kabla sijafungua biashara mpya, maana kuna kauli za kisiasa na sheria zilizopo vinanichanganya.
Ikumbukwe, mwaka 2023 ilitoka kauli kutoka kwenye serikali ya Samia kuwa wafanya-biashara wapya watapewa muda kufanya biashara kwa kipindi cha miezi 6 mpaka mwaka 1 bila kutozwa kodi.
Sasa, kuna mtu nafahamiana naye yupo Maisapaa nilimtafuta ili kumuuliza taratibu na gharama za kupata leseni ya biashara ninayotaka kufungua, akaniambia niende miezi 3 baada ya kufungua biashara.
Maana yake, baada ya miezi mitatu niende TRA nikiwa na TIN, mkataba wa pango na barua ya utambulisho, ili nipate Tax Clearance, ndiyo niende Manispaa/Tausi Portal kwaajili ya leseni.
Sasa, wasiwasi wangu ni kwamba ndani ya hii miezi mitatu wazee wa tai mbele wanaweza kuvamia ofisini na wakikuta sina vibali inaweza kuleta shida japokuwa tayari kuna matamko ya kisiasa na sheria ambazo hazipo wazi kwa wafanya-biashara.
Naomba ushauri wenu wazoefu au ambao mna taarifa zaidi ya hizi nilizonazo mimi.