Vibaka watikisa Dar

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
vibaka katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam limekuwa tishio kwa wananchi eneo hilo. Wimbi hilo linasemekana kutishia upitishwaji wa magari yanayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi za jirani na kuliweka eneo hilo katika hali ya wasiwasi.

Eneo linalolalamikiwa zaidi ni katika daraja la Ubungo linalopakana na mitambo ya Shirika la Umeme (Tanesco) katika pande zote vibaka hao wamekithiri kwa kukwapua vioo vya pembeni ya gari (side mirror) hasa ambavyo havijawekwa alama, simu za mkononi na mikoba ya akinamama. Inasemekana kuwa vibaka hao wana utalaamu wa hali ya juu wa kuchomoa vioo hivyo kiasi cha madereva wengi kushindwa kuwadhibiti.

“Mimi waliniambia hivi karibuni nilipokuwa kwenye foleni maeneo hayo. Nilishtukia tu vijana wawili wamesimama pande mbili za gari yangu. Mara nikashtukia vioo havipo na wale vijana wametoweka,” alisema mmoja wa madereva ambaye ameathirika na wizi huo.

Dereva huyo alisema madereva wengi wanaopitisha magari yao kutoka bandarini hulazimika kuvifunga vyoo hivyo kwa gundi ya karatasi ili visichomolewe. Grace Martin alisimulia jinsi baba yake mdogo mwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser (Prado) lilivyochomolewa vioo katika eneo hilo.

“Tulikuwa kwenye foleni, mara wakaja vijana wawili, mimi sikuwashtukia kwa sababu kulikuwa na msongamano wa magari nikadhani ni wapiti njia. Ghafla wakachomoa vile vioo. Baba alishtuka hakuamini macho yake. Akatoa bastola yale lakini tayari vijana wale walishatoweka,” alisema Grace.

David Matiko ambaye ni dereva teksi katika eneo hilo anakiri kuwepo kwa uhalifu katika eneo hilo, na kuongeza kuwa eneo hilo halipitiki wakati wa usiku. “Hapa mchana wanakwapua simu na vifaa mbalimbali vya abiria. Usiku ndiyo hapapitiki kabisa. Juzi kuna rafiki yangu kapita saa tano usiku akaporwa kila kitu hapa,”alisema Matiko.
Mtandao wa vibaka na wapiga debe Ubungo Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa wa vibaka na wapiga debe eneo la Ubungo unaoratibiwa kwa ushirikiano wa karibu na jeshi la Polisi. Kundi la kwanza za vibaka hao ni wale wanaofanyia kazi katika Daraja la Ubungo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, vibaka hao wanajulikana hata na wafanyabiashara wa soko lisilo rasmi katika eneo hilo, lakini ni hatari mno kuwataja. “Hao vibaka wanajulikana na mara nyingi hucheza kamari mchana katika eneo hilo. Ukiwataja ndiyo utakuwa mwisho wa kufanya biashara yako hapo”.

Chanzo hicho kinaendelea kubainisha kuwa kuna askari polisi anayeratibu utendaji wa vibaka hao na anajulikana (jina tunalo). “Huyu askari huwa anakuja eneo la Ubungo karibu na mataa kila Jumamosi kuchukua mgao unaotokana na mauzo ya vitu vilivyoporwa na vibaka.

Kibaka asipopeleka ndiyo unakuwa mwisho wake wa kufanya kazi eneo hilo”. Chanzo hicho kinasema kuwa mara nyingi vibaka hao wakishaiba hukimbilia upande wa pili wa daraja (kuelekea Kibo) ambako kuna maduka na baa na hapo ndipo mauzo na mikakati hupangwa.

MatemboHili ni kundi la pili ambalo linajihusisha wababe walioajiri wapigadebe ambao pia ni vibaka. Kati ya vigogo wa kundi hilo wanatajwa wanne maarufu na hatari zaidi (Majina tunayo).Kundi hilo limeonekana kuwa na mizizi mirefu, likilihusisha jeshi la polisi kwa kujua au kwa kutokujua.

Awali kundi hili lilikuwa likimilikiwa na wababe kadhaa ambao wameajiri wapigadebe katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukusanya mapato kwa siku. Kwa mujibu wa chanzo chetu, biashara hiyo haramu inawaingizia fedha nyingi hata kuwawezesha wababe hao kumiliki majumba makubwa maeneo ya Mbezi, Kimara, Ubungo na sehemu nyingine.

Wababe hao pia wanamiliki magari ya abiria na pikipiki. “Wanchokifanya ni kugawana vituo vya daladala na zamu za kuchukua mapato kutoka kwa wapigadebe waliowaajiri. Kila mpiga debe kwa siku anatakiwa atafute hesabu ya Sh 15,000 na utakuta mbabe mmoja kwa siku anakusanya hadi Sh 500,000," kilieleza chanzo chetu na kuongeza:
" Akishazipata hutoa mchango wa chama, mgawo kwa vituo vya polisi Mbezi, Kimara, Ubungo (Bus terminal) na Urafiki. Kilichobaki ndiyo anachukua yeye.” Mbali na kukusanya mapato kwenye vituo vya daladala, genge hilo pia hukusanya ushuru wa Sh1,000 kila siku kwa kila mfanyabiashara aliye ndani ya eneo la kituo cha daladala cha Ubungo na wale walio kando ya Tanesco.

Pia waendesha pikipiki (bodaboda) wanaoegesha maeneo hayo hulipishwa Sh1,000 kila mmoja kwa siku, mfanyabiashara anayekaidi kutoa fedha hizo hupelekwa kwenye kambi ya mateso iliyotajwa kwa jina la“Mason Beach” iliyoko kando ya mto Ubungo barabara ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Mateso yanayotolewa huko ni makali mno ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nguo, kupigwa na wababe hao waliokubuhu katika mafunzo ya karate. Ndiyo maana madereva wengi wanawaheshimu wapiga debe,” kinaeleza chanzo hicho. Kambi hiyo inadaiwa pia kutumika kuwatesa watu wanaoonekana kutishia uhai wa genge hilo au wanaogoma kutoa fedha pale wanapokabwa na vibaka.

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Japhet alikiri kulifahamu kundi la Matembo lakini akadai kuwa kwa sasa kundi hilo limedhibitiwa na baadhi yao wahalifu wamepelekwa mahakamani. “Kwa sasa hali imetulia. Kuanzia Januari 2011 tumejitahidi kuweka ulinzi shirikishi na tumeweka vijana wenye sare wanaosimama kila baada ya mita 50,” alisema. Japhet alibainisha kuwepo kwa mkakati wa kumaliza uhalifu Ubungo kwa kutaja taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama International Centre and Network for Information on crime Tanzania (Icnic- TZ).

Alisema kuwa taasisi hiyo ya kimataifa imejikita kwenye miji yenye uhalifu duniani ambapo kwa sasa inahudumia nchi za Brazil na Tanzania. Kwa Tanzania inafanya kazi jijini Dar es Salaam kwenye maeneo sugu kwa uhalifu ya Ubungo na Keko.

Alipoulizwa kuhusu kuendelea kwa uhalifu katika eneo hilo licha ya kuwepo kwa Icnic na walinzi shirikishi, Japhet alisema hana uhakika kama jitihada hizo zimefanikiwa vya kutosha, “Sina uhakika kama tumefanikiwa vya kutosha, lakini tutaendelea kufuatilia kama bado kuna malalamiko ya wizi,” alisema. Mmoja wa viongozi wa Icnic, John Lubuva alisema taasisi yao imefanya jitihada kubwa ya kuhamasisha ulinzi shirikishi kwa kufaya tafiti na mikutano na wananchi.

“Kwanza tulifanya utafiti katika maeneo hayo, kisha tukawashauri wananchi waunde vikundi vya ulinzi na sisi tumevijengea uwezo wa kufanya kazi,” alisema Lubuva. Hata hivyo, Lubuva aligusia kuwepo kwa soko katika eneo hilo kuwa ndiyo kunachangia uhalifu, “Pale kuna soko na wananchi wenyewe walisema kuwa ndiyo linachangia. Sisi hatuwezi kulihamisha hilo soko, ni mipango ya halmashauri,” alisema Lubuva.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kundi la Matembo sasa linatumia vijana hao kupora kisha kuwakamata mtu huyo aliyeporwa na kumpeleka polisi wakisema kuwa ndiye mwizi huku wakijifanya wao wema machoni pa polisi. Mwenyekiti wa Mtaa wa Ubungo Kisiwani, John Ndimbo alisema amejitahidi kuimarisha ulinzi katika eneo hilo lakini, kwa kuwa lina watu wengi na kuhusisha viongozi wengi ni vigumu yeye peke yake kuwajibika.

“Lile eneo (Ubungo darajani) limegawanyika katika mitaa mitatu. Kuna Ubungo Kisiwani, kuna Kibo na Kibangu. Tunafanya ulinzi kwa kushirikiana na polisi na hata wakati mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni huja kukagua. Lakini ni kweli malalamiko ya wizi bado yapo kwa kuwa hilo ni eneo kubwa na lina watu wengi,”alisema Ndimbo.

Ndimbo amelalamikia kuwepo kwa soko lisilo rasmi katika eneo hilo akidai kuwa ndiyo chanzo cha kufurika kwa vibaka katika eneo hilo. “Kamati yetu ya maendeleo ya Mkoa ilishauri kuondolewa kwa soko hilo lakini hatuna uwezo wa kufanya hivyo. Mwenye uwezo ni Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni”. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Raphael Ndunguru kila alipopigiwa simu kuzungumzia suala hilo aligoma akidai kuwa yuko kwenye kikao nyeti.

“Niko kwenye kikao, nipigie baada ya saa moja” alisema na kukata simu. Baada ya saa moja Ndunguru aliendelea kukwepa akisema,“kwani, unataka kuzungumzia nini?. Kwa sasa niko kwenye kikao nyeti, siwezi kuzungumzia suala hilo.” Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Sebastian Masinde ameeleza kutokuwa na taarifa ya uhalifu huo kwa kuwa hakuwa ofisini kwa muda mrefu. “Mimi nimekaimu tu ofisi, kamanda mwenyewe hayupo. Nashukuru kwa kuwa umenipa taarifa na mimi nitaifanyia kazi,” alisema Masinde.
 
Dalili za failed governance na organized crimes. Mwishoe itageuka Mafia top-down bcoz these criminals will only get greedier and not otherwise.
 
Laiti wananchi wenye magari wangehamasishana kununua vifaa vipya madukani na kuachana kabisa na mambo used wizi huu ungepungua kwa kiasi kikubwa au ungekwisha kabisa......wanakwapua kwasababu soko la uhakika lipo.........
 
Binafsi tatizo si kwa wenye magari kununua vifaa vipya sababu hata hivyo vipya siku hizi vimechakachuliwa kutokana na kushamiri kwa biashara huria watu wanaingiza bidhaa ambazo hazina ubora (wanaita za mchina) hivyo inawalazimu watu kununua vipuri vilivyotmika sababu ni vipya ingawa vingi vinaibiwa mtaani.

La msingi ni jukumu kwa wananchi wote kuanza kuwadhibiti watu hawa wanaoleta tabia mbaya hizi za wizi, binafsi nadhani tuchukue wenye sheria mikononi sababu wanadora waliopewa kazi nao wanashirikiana na wahalifu, leo wamkamata mtu wampeleka kituoni lakini baadaye wanamwachia sasa tuweke pembeni mambo ya sheria za haki ya binadamu sababu tukitumia sheria ya jino kwa jino wizi huu kwa kiasi fulani utapungua, mfano mtu akikwapua simu au kitu chochote tukate mkono au mguu sababu tukianza kwa watu na wakaona hali hiyo hakika tutajaribu kupunguza uhalifu huo, lakini tukisema HAKI ZA BINADAMU tunarudi nyuma.
 
mi naona akikamatwa ni moto tu au kama una bastola ifanye kazi yake ndo sululisho la wanaorudisha maendeleo nyuma..
 
Kama serikali imeshindwa kuweka ulinzi sehemu hiyo, mbunge wa Ubungo unangoja nini? ndio points hizo, hapo wanapita watu wa kutoka kila sehemu ya nchi, na pia wa nchi jirani. Mbunge, fanya vitu, hapo ndio pa kujitangaza umahiri wako na vipi unaweza kusaidia wananchi. Na kama utakaa kimya, tutauliza, mbunge vipi, pamekushinda?
 
Jamani mbona wanahatarisha usalama barabarani?? sasa ukimkwapulia mtu side mirror unategemea aendeshe vipi kiusalama?? kweli ujinga ni chanzo cha umaskini. Ndio maana vibaka wanachomwa moto manake this is too much.

Inabidi tutembee na bastola, akikusogelea tu kuiba kioo unamshoot nadhani itakomesha swala hili la wizi wa vifaa vya magari kwenye foleni.
 
Dawa ya kufuta wizi wa side mirrors ni kujenga flyovers na kufuta kabisa foleni pale ubungo. Kulifuta kundi la kimafia hapo kunahitaji juhudi za polisi wanaofanya kazi zao. :smow:
 
Laiti wananchi wenye magari wangehamasishana kununua vifaa vipya madukani na kuachana kabisa na mambo used wizi huu ungepungua kwa kiasi kikubwa au ungekwisha kabisa......wanakwapua kwasababu soko la uhakika lipo.........

Sawa kabisa..tatizo kwenye maduka hayo zimejaa spare za kichina..hizi biashara za kishenzi shenzi zingepigwa marufuku tu..angalia biashara ya chuma chakavu inavyosababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu!!
 
Back
Top Bottom