gasper kolila
Member
- Oct 26, 2009
- 16
- 0
Kuna jamaa wawili walichelewa kurudi makwao, sasa ilipofika usiku mkubwa, ikabidi wakubaliane kuondoka usiku huohuo kwa kupitia njia ya mkato ya maeneo ya makaburini, Walipofika maeneo ya makaburi wakamkuta mtu anakimbizwa na vibaka, ikabidi watumie mbinu ili wale vibaka wasiwadhuru,
JAMAA 1. Akamuuliza mwenzake" kwani wewe ulikufa lini?
JAMAA 2 Akajibu mimi nilikufa mwaka jana na kaburi langu ni lile pale chini ya ule mti mkubwa paleeeeee.
JAMAA 1. Akamwambia twende unipeleke nikalione, ndipo wakaanza kuelekea upande huo ambao kumbe vibaka walikuwa wamesimama wakiwasikiliza tokea mwanzo. walivyokuwa wanawasogelea , jamaa 1 akauliza na hawa jamaa hapo mbele unawafahamu?
jamaa 2 akajibu hebu tuwaulize kwanza, wale vibaka walivyosikia ilibidi watimue mbio za mwaka kwani waliweza kuvunja hata misalaba ya baadhi ya marehemu waliopumzika kwa raha mavumbini,
Hapo yule aliekuwa anakimbiza kumbe alikuwa amejificha karibu kabisa na wale jamaa wawili, ilimbidi kukimbia tena akiwafata wale vibaka, kwa salama yake kwani yeye alikuwa pekeyake.......