Viazi vitamu vyadaiwa kuzalisha mapacha

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Umeshawahi kutamani kupata watoto mapacha?. Basi taarifa hii inaweza ikawa njema kwako.

Ulaji wa viazi vitamu kwa kipindi kirefu unadaiwa kusaidia uzalishwaji wa mayai mengi kwa Mwanamke na hivyo kupelekea kupata watoto mapacha.

Jiji la Igbo-Ora lililopo nchini Nigeria ni jiji lenye mapacha wengi na Nigeria imepewa jina la mji mkuu wa Mapacha Duniani kwa kuwa na watoto mapacha wengi zaidi kuliko eneo lolote duniani huku viazi vitamu vikiliwa zaidi nchini humo.

Viazi vitamu vinatajwa kuongeza homoni aina ya โ€˜phytoestrogenโ€™ ambayo huchangia kwenye kupevusha yai zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Utafiti wa kisayansi bado unafanywa ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

Chanzo: TBC Online
 
Story inayoendana na hii niliisoma ikihusu state ya Igbo-Ora. Huko Nigeria
Huko kuna mapacha wengi sana inasezekana Wakazi wa huko wanakula sana magimbi hivyo kusababisha wanawake wa huko kuzaa sana mapacha
 
Sio Kweli, kwetu vijijini tulikula Sana hayo makitu ila kwa kipindi chote nilichokuwepo vijijini kamwe sikuwahi on a wanawake wakijifungua mapacha.

Ilikuwa nadta Sana kuona watoto mapacha wanazaliwa kijijini kwetu
 
Back
Top Bottom