Viapo vya ndoa havitekelezeki

Viapo vya ndoa havitekelezeki

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
150305111330_talaka_viapo_512x288_bbc_nocredit.jpg

Harusi na viapo visivyotekelezeka.

Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya. Lakini kwa muujibu wa utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe .

Mtafiti uliofanywa kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema.Ukilinganaisha na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki kuwa mgane ama mjane.

Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao wameumbwa kutoa huduma katika familia zao nah ii inamaanisha kwamba wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi ya muda mrefu,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili.

Walifanyiwa utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili.Miwili ndani ya utafiti uliofanywa kwa miaka ishirini.Asilimia thelathini na mbili ya ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.

Kikosi cha utafiti kiliongozwa na amelia Karraker, ambaye ni profesa msaidizi juu ya masuala ya maendeleo ya binaadamu na utafiti juu ya familia kutoka katika chuo cha Iowa State University.Analinganisha matukio ya namna nne kansa,magonjwa ya moyo,kiharusi na magonjwa ya njia ya hewa kwa wanawake na wanaume na matokeo ya ndoa.

Tamu na chungu ya ndoa Utafiti huo umebainisha kwamba , kuna tofauti ya kujisikia mgonjwa sana na huwezi kupika chakula cha jioni, ama unahitaji mtu hasa wa kukulisha masuala haya yanaweza kubadili upepo ndani ya ndoa .

Katika hali hiyo,utafiti huo hauoneshi dhahiri kuwa mume ama mke anadai talaka,takwimu kamili zinaonesha kwamba wanawake ni wepesi zaidi kuomba talaka kuliko wenza wao.

Bi Karraker anasema amegundua kwamba kwamba inawezekana baadhi ya wanawake ambao huachwa kwasababu ya huduma zao ama kushindwa kuhudumia.Tafakari juu ya uhai ama kifo husababisha watu wajitafiti wenyewe na kujiuliza maswali muhimu kuwa ni nini muhimu maishani mwao? Anaeleza mtafiti huyo.

Wanawake wakati mwingine huribuka kwa kusema kuwa waume zao hawawajali,na hawafurahishwi na suala hilo ama husema sikufurahishwa na mwanzo wa mahusiano yao, na wansema kwamba wako radhi kubaki peke yao kuliko kujitosa katika ndoa isiyofaa.



CHANZO:BBC
 
TALAKA KATIKA UKRISTO (Mst. 6-8) – Hakuna
talaka katika ukristo. Mwanadamu YEYOTE iwe ni
Mchungaji, Askofu, Jaji wa Mahakama Kuu ya
Rufaa au yoyote hana ruhusa kumtenganisha
mtu na mkewe, na cheti chochote cha talaka ni
batili, hakitambuliwi na Mungu. Mungu
alichukuliana na watu wa Agano la Kale kwa
ugumu wa mioyo yao, lakini hachukuliani na
yeyote katika Agano Jipya kwa suala la talaka.
Hata kama mke ameachwa kwa talaka potea,
hana ruhusa kuolewa na mwingine (1
WAKORINTHO 7:10-11).KUMWACHA MKE KWA
SABABU YA UASHERATI (Mst. 9) – Hiki ni
kisingizio cha watu wengi wasio na maarifa
kuwaacha wake zao. Nyakati za Biblia mtu
alipotoa posa kwa mchumba wake, hata kabla
hawajaoana, waliitwa mtu na mkewe
(KUMBUKUMBU 22:23-24; MATHAYO 1:18-20).
Katika uchumba, kama mke huyo alithibitishwa
kuwa amefanya uasherati kwa kuwa na mimba
au vinginevyo ilikuwa ni halali kumwacha maana
ni dhahiri kwamba siyo mwaminifu. Ni kwa
sababu hiyo Yusufu alitaka kumwacha Mariamu
kwa kudhani alifanya uasherati. Vivyo hivyo,
katika Kanisa, watu ambao bado ni wachumba,
hata kama posa imekwisha kutolewa;
mmojawapo anapothibitika kuwa amefanya
uasherati, huyo mwenzake ana ruhusa ya
kumwacha kwa sababu inadhihirisha kwamba
hajaokoka. Lakini mtu na mkewe wakiisha
kuoana, uzinzi siyo sababu ya kuwaruhusu
kuachana. Mume anapaswa kumsamehe mkewe
mara saba mara sabini makosa YOTE kama
Mungu katika Kristo alivyotusamehe sisi. Je,
tulisamehewa dhambi zote kasoro uzinzi? Jibu ni
la! Basi uzinzi siyo kisingizio cha kumwacha mke
(WAEFESO 4:32).
 
Wow yaani akaliwe huko nisamehe wakati mimi ni mwaminifu. Kweli kuwa kondoo ni taabu inatakiwa uwe kondoo kwelikweli.
 
Back
Top Bottom