Ni nani kichaa?
Marekani ambaye aliipiga miji ya Hiroshima na Nagasati huku akijua anauwa maelfu ya raia wasio na silaha, amewaunga mkono madikteta na wauaji wengi wa Afrika, ameuwa malaki ya wa Iraq wasio na hatia, ameendelea kuua maelfu ya raia wasio na hatia Afghanistan, ameibadilisha Libya kutoka nchi ya asali na maziwa kuwa nchi ya mauaji, majuto na laana zote huku akiiba mafuta.
Israel Imekuwa na silaha za nyuklia peke yake mashariki ya kati, imepora ardhi ya wapelestina wasio na silaha, imekuwa ikiwauwa waPalestina wasio na silaha kwa kutumia mabomu ya sumu ambayo hayakubaliki duniani, imewahi kuzishambulia nchi kama Syria, Sudan na Iraq kwa kuhisi tu wanatengeza silaha kali, na hivyo yaweza shambulia nchi yoyote duniani kwa kuhisi tu.
Iran haijawahi ivamia nchi yoyote duniani wala kuua watu ovyo. Je kwa kutengeneza nishati ya nuklia tu ni tishio?
,