Vazo ya Niqab haramu Ufaransa.

Vazo ya Niqab haramu Ufaransa.

Patrick Elias

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
332
Reaction score
108
Vazi ya Niqab haramu Ufaransa

Mahakama ya haki za binadamu barani Ulaya imeamrisha kuendelea kutekelezwa hukumu ya kupiga marufuku vazi la hijab linalofunika uso mzima nchini Ufaransa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na nne raia wa Ufaransa ambaye alidai kuwa marufuku hiy inakiuka haki zake za kuabudu na kujieleza.
Mahakama hiyo hata hivyo imsisitiza kuwa Ufaransa inayo haki ya kuhifadhi utangamano na usawa katika jamii kwa kuweka marufuku hiyo.
Sheria hiyo iliwekwa nchini Ufaransa miaka minne iliyopita na tangu hapo Ubelgiji imeiga.

http://www.bbc.co.uk/swahili/medianuai/2014/07/140702_niqab_ufaransa.shtml
 
Kweli wana haki kufanya hvyo kwani ata ukienda nchi za kiislam ni marufuku mwanamke ata nywele kuonekana bila kujali dini yako.
 
Pepo haiedwi kwa mavazi, bali kwa
matendo yako, machangudoa wa
mchana wengi hutumia vazi hilo
kwenda gest, yani limegeuka vazi
la gesti, huku wenngine wakisema
ni vazi la hesma, hata majambazi
sku hizi hulitumia kuibia.... Hata
shekhe fulani hulitumia kutoroka
pale anaposakwa na polis
 
Kweli wana haki kufanya hvyo kwani ata ukienda nchi za kiislam ni marufuku mwanamke ata nywele kuonekana bila kujali dini yako.

Tofauti na nchi ya Saudia na Iran nchi gani yenye hiyo sheria unayosema wewe?

Vp style kama hizo ?
 
Attachments

  • 1404292136792.jpg
    1404292136792.jpg
    49.9 KB · Views: 82
Tofauti na nchi ya Saudia na Iran nchi gani yenye hiyo sheria unayosema wewe?

Vp style kama hizo ?

Hizo hizo ulizotaja kwani kila nchi ina sheria zake na ukikubali kwenda kwao sharti uzifuate,hautaki rudi kwenu au tafuta nchi nyngne ya kuishi ambayo haina sheria uipingayo.
 
Kweli wana haki kufanya hvyo kwani ata ukienda nchi za kiislam ni marufuku mwanamke ata nywele kuonekana bila kujali dini yako.

Tofautisha kujisitiri na kuvaa nikab nadhani wanawake wa kiislam tukivaa mavazi ya kujisitiri sio lazima nikab
 
Tofautisha kujisitiri na kuvaa nikab nadhani wanawake wa kiislam tukivaa mavazi ya kujisitiri sio lazima nikab

Cha muhimu kufuata sheria ya nchi,ukiona ngum unarudi kwenu kwani waislam ambao ni wazawa wapo kimya,pili lazima kuwe na sababu za msingi kwa marufuku hyo ,je wewe unazijua?
 
Cha muhimu kufuata sheria ya nchi,ukiona ngum unarudi kwenu kwani waislam ambao ni wazawa wapo kimya,pili lazima kuwe na sababu za msingi kwa marufuku hyo ,je wewe unazijua?

uvaaji wa nikab unaficha mambo mengi ya ajabu hata sehemu kama za university nchi za kiarabu huruhusiwi kuingia maeneo hayo ukiwa umevaa nikab
 
hata kama watapiga marufuku niqaab,uislam utadhihiri hata kama makafiri watachukia......
 
Niqab is outlawed in Azerbaijan,Tunisia and Turkey where majority of the population is muslim.IT is nearly impossible to find work if you wear niqab.
Source:niqab Wikipedia
 
Back
Top Bottom