Vannesa amfungukia live Jack Cliff

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Baada ya kumkwapua Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ aliyekuwa mpenzi wa modo Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’ kisha modo huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ameibuka na kumzungumzia ‘mtalaka’ huyo wa Jux.

V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack.

Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.

“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.

Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposika amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:

“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria.

“I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”

Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.

Chanzo: GPL
 
Yani Vanessa kiboko ya wachochezi....hahhahahahahahaahahahah
 
Katoa jibu lenye kuziba mianya ya maswali mengine kwa leo ina tosha,msimuulize tena ndo mkome umbeya, halafu acha umbea
 
Wanashauriana vibaya sana hawa watoto huyu Jack nimesoma mahala baba yake mzazi ni raia wa UK badala ya kwenda ubalozi wao kudai mkoba wake alikotoka baba yake au makazi ya kudumu kama anataka abaki na passport ya Tanzania choices ambazo ni haki yake kisheria za UK akaenda kupiga box huko kuliko kubeba madawa ya kulevya.
 
honestly jux anaendana zaid na jack and not vanessa, walipendezana zaidi, pia jack ni mzuri kuzidi vanessa tena kwa mbali sana. pia hukumu ya jack ilishatolewaga ni miaka sita only then anatoka. ahsante.
 
Baada ya kumkwapua Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ aliyekuwa mpenzi wa modo Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’ kisha modo huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ameibuka na kumzungumzia ‘mtalaka’ huyo wa Jux.

V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack.

Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.

“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.

Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposika amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:

“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria.

“I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”

Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.

Chanzo: GPL
Anaitwa Juma Mussa Mkambala siyo Juma Mussa Mpolopoto
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom