Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Katika karne hii ya 21, vita vya kiuchumi havipigwi tena kwa silaha wala bunduki, bali kwa mitaji, hisa, na ushawishi wa kifedha. Katika anga hiyo, kuna mapacha mawili waliojitokeza kwa nguvu ya ajabu: Vanguard Group na BlackRock Inc.
Haya si makampuni ya kawaida – ni taasisi za usimamizi wa mali (asset management) ambazo zina ushawishi wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja katika maamuzi ya biashara, sera, na hata siasa za kimataifa.
Ripoti ya Financial Times ya mwaka 2023, Vanguard inasimamia zaidi ya $8 trilioni katika mali duniani kote, huku BlackRock wao wakiwa juu zaidi kwa takribani $10 trilioni. Hii inamaanisha kuwa viongozi wa taasisi hizi – kama Salim Ramji (ambaye ndo Mkurugenzi Mkuu mpya wa Vanguard) na Larry Fink (Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa BlackRock) – wana nafasi kubwa ya kuathiri uchumi wa dunia kuliko hata baadhi ya marais wa mataifa.
Direct Influence dhidi ya Indirect Influence
BlackRock na Vanguard si tu wanamiliki hisa kwenye makampuni makubwa kama Apple, Microsoft, Coca-Cola, Pfizer, pamoja na Google, bali pia wana nafasi katika taasisi za fedha, bima, uzalishaji wa vyakula pamoja na vinywaji, nishati, na mawasiliano.
Ripoti ya **Bloomberg ya mwaka 2022 ilionyesha kuwa makampuni haya mawili yalikuwa miongoni mwa wamiliki wakuu wa hisa katika zaidi ya asilimia 80 ya makampuni yaliyoorodheshwa kwenye S&P 500 – orodha ya makampuni makubwa zaidi ya kibiashara nchini Marekani.
S&P 500 ni kifupi cha Standard & Poor 500 ikiwa ni namna stock market index ama geresho ambalo hutumika kutazama ufanisi na utendaji kazi wa makampuni 500 makubwa ndani ya Marekani. Sasa chukulia picha wajomba hawa wawili wana jumla ya asilimia zaidi ya 80 kwenye makampuni yaliyopo kwenye S&P 500.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na Said Salim Bakhresa kuwa na ushawishi kwa viwanda vyote vya chakula na maduka makubwa ambayo yanauza bidhaa muhimu kwa wafanyabiashara wa rejareja, kushoto awepo Ghalib Said Mohamed ambaye yeye ndio mwenye ushawishi katika benki zote zaidi ya 45 zilizopo nchini, na upande wa kulia unakutana na Mohammed Dewji kushika usukani wa sekta ya usafiri na mawasiliano.
Kwa mfano huu, si vigumu kuelewa kwanini wataalamu wa uchumi kama Nomi Prins katika kitabu chake “Collusion: How Central Bankers Rigged the World” wanaeleza kuwa nguvu ya taasisi hizi kuwa ni nguvu kubwa iliyopo gizani ila inafanya kazi kubwa sana, ni sawa na kusema kuwa hawa jamaa ni “serikali isiyo rasmi ya kifedha duniani”.
Baina ya hawa mapacha wawili kuna watu ambao ndo wanaonekana ndio Masterminds na wasuka mipango wakuu wa sera na mipango. Mfano, Supermaket kubwa duniani kama Walmart, Costco, Kroger pamoja na Target, hawa wanne pekee hawakoromi mbele ya Blackrock wala Vanguard.
Dunia ilipata wasaha wa bwana mmoja kuandika kitabu cha The Hidden Power of Passive Investing ambapo alielezea kwa undani mbinu na mikakati ya hawa mapacha wawili ambao siku wakiamka vibaya kuna watu wataimba haleluya.
Msumari wa moto mwingine ni kutoka kwa John Train ambaye kitabu chake ukiwa sio timamu vya kutosha unaweza kusoma karatasi mbili tu na ukahamia kusoma magazeti, kitabu cha The New Money Masters kimedadavua kwa undani namna ambavyo kuna watu wanaheshimika kuliko hata mawaziri wakuu na wakiingia sehemu unakutana na ukimya wa hali ya juu sana.
Dotto katika uongozi wa BlackRock kuna watu nane waliounda kampuni hiyo mnamo 1988, wakiongozwa na Larry Fink. Leo, BlackRock inatoa ushauri wa kifedha kwa benki kuu kubwa duniani kama Federal Reserve, Bank of England, pamoja na European Central Bank.
Kwa upande wa kulwa ambaye ni Vanguard, yeye amepata Boss mpya, Salim Ramji ni jina jipya lakini lenye ushawishi mkubwa, akiwa ni mtaalamu wa uwekezaji aliyeongoza pia idara ya ETFs ndani ya BlackRock kabla ya kuhamia Vanguard. Kabla ya kuwa boss, Salim Ramji alikuwa akisimamia idara ya Mfuko wa Uwekezaji ambayo pia idara hii hujulikana kama iShares.
Huyo bwana mkubwa alikuwa akisimamia biashara ambayo thamani ya mali zake ilikuwa ni zaidi ya dola Trilioni 3 za kimarekani, sio pesa za Kitanzania, ni Trilioni 3 pesa za Marekani, sawa na Quadrilioni 7.8 za kitanzania ama kwa lugha nyepesi ni Trilioni elfu saba na mia nane.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka The New York Times ya mwaka 2024, kampuni hizi zimekuwa zikikabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wanaharakati na wanasiasa kutokana na ushawishi wao mkubwa katika mwelekeo wa dunia – kuanzia mabadiliko ya tabia nchi hadi usawa wa kijinsia na vipato vya wafanyakazi wake.
Baadhi huona kuwa kwa sababu BlackRock na Vanguard huwekeza katika makampuni yanayoshindana, wao huweka utulivu wa kibiashara badala ya ushindani – jambo ambalo linapingana na misingi ya soko huria.
Mbali na vitabu vya Nomi Prins, kitabu cha “The New Confessions of an Economic Hit Man” cha John Perkins kinaeleza jinsi mashirika ya kimataifa yanavyoweza kutumia fedha kama silaha ya kisiasa. Hii inaakisi moja kwa moja jinsi Vanguard na BlackRock wanavyoweza kutumia mitaji yao kuathiri maamuzi ya serikali na mashirika makubwa.
“The BlackRock Story” na “Trillions: How a Band of Wall Street Renegades Invented the Index Fund” vilivyoandikwa na Robin Wigglesworth, vinachambua historia ya taasisi hizi na jinsi zilivyoteka ulimwengu wa fedha bila kelele nyingi wala fujo bali ni pesa na akili nyingi.
Je, dunia iko salama mikononi mwa watu wachache wenye mabilioni ya dola, au tunakabiliwa na aina mpya ya ukoloni wa kifedha?