Vanessa Mdee ni mwanakulitaka na amelipata

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph
.
Kwanza kabla ya yote nieleze masikitiko yangu na kuonesha kuhuzunishwa kwangu, na mambo aliyoyasema Dada na Msanii wetu Vanessa Mdee juu ya namna ambavyo wasanii wakike wanahaha ili kukidhi mahitaji Yao, Pole Sana.

VMoney tumeona malalamiko yake akidai Kwamba mziki wa ni biashara ambayo haina faida hasa kwake kila siku anafanya kilekile, Japo sijui alimaanisha mafanikio gani.
.
VMoney anasema alikuwa akifake Maisha, akitumia gharama kubwa Sana lakini kinachorudi ni Kidogo, hakuna ambaye alimlazimisha Vanessa aishi Maisha ambayo ni tofauti na uhalisia wake ni yeye aliamua kuishi hivyo kutokana na Brand aliyokuwa nayo kama Msanii kama ilikuwa na gharama angeishi kawaida, bado angebaki kuwa VMoney.

VMoney anasema mziki hauna faida, ikumbukwe V amefanya muziki Kwa zaidi ya miaka 7, hapo katikati amepata Deals (DOFFI, EAGT Universal NK), ameanzisha Lebo ya Mdee Music aliyomsaini mdogo wake MimMars na Msanii wake anafanya muziki mzuri, VMoney pia alianzisha Love & Money Tour ambayo alifanya katika baadhi ya mikoa Bongo, ameshiriki kwenye tuzo nyingi sana za nje ya nchi MTV, AFRIMMA NK.

VMoney anasema mziki ulikuwa haumlipi inanikumbusha wale watu waliokuwa wakimlalamikia Marehemu Boss Ruge kusababisha wao kukwama kimaisha nakumbuka wakati mmoja akijibu madai hayo alisema tatizo wasanii wetu huwa hawajiandai Maisha baada ya muziki, akisema Maisha ya muziki ni kama kusoma kitabu ukishasomwa na Mashabiki unawekwa Pembeni anasomwa mwingine hivyo wanasahau kila siku vipaji vipya vinatoka na mashabiki wanataka wapya sasa hichi ndiyo kilimkuta VMoney navyodhani Mimi na asilalamikie Tasnia ajilaumu mwenyewe.
.
Inaonesha licha ya Exposure alizopata lakini alifanya muziki bila malengo (Hana Direction) angekuwa na malengo Kwa aliyoyafanya 2015 - 2019 nadhani sasa asingekuwa mtu wa kulialia.

Ukimsikiliza VMoney unagundua kuwa alijua atafanya muziki maisha yote hivyo hakuwekeza kwenye kitu chochote nje ya muziki, wakati angeweza kutumia muziki kuwekeza kwingine (Diamond, Jux, Shilole nk wamefanya) Yaani V ameshindwa hata kufungua Duka la heleni kupitia muziki.

Shishi Baby huyu Msanii na Mama Ntilie mbona hatujawahi msikia akilialia kuhusu muziki wa wanawake ni kwa sababu alijua anatafuta nini kwenye mziki ndiyo maana alipopata mara moja tu akaja na Shishi Food na inamuingizia Pesa bila kudanganya, Komando Jide kapambana sana mpaka bado yupo hajawahi kuliakulia.
.
Mimi kwangu Vanessa ni Mwanakulitaka Mwakulipata nadhani kuanguka kwake kimuziki nilianza kupaona pale alipoanzaga kutengeneza Kiki na Shilole wakagombana Kwa Kingereza baadaye wakasema ilikuwa Maigizo Tu.

Navyodhani Mimi Sangu J Kwa sasa VMoney amepata tulizo Tu la Moyo Kwa Shemeji Rotim baada ya kutengana na Mtanzania Mwenzetu na amefanya maamuzi ya kuzungumza akiwa na furaha sana hivyo tumuache wakati furaha ikiwa Standard atarudi kawaida Tu Kwa sasa tumuache.

Kilichonifanya niandike Haya ni kwasababu Maneno yake nimeona yanawavunja Moyo wasanii wengi hasa chipukizi na waliopo kwenye Industry , haiwezekani watu wanapambana wewe unawaambia huwa Mnafake hii kwangu niliona haijakaa poa Bora angekaa kimya kama alivyofanyaga Japo tulimmiss Sana.
.
FB : Insta : Twit : Sangu Joseph
.
#KijanaMzalendo #IloveTZ

Tazama :
 
Maisha ni kupambana. Au yeye alidhani itakuwa mteremko tuu,, hakuna kitu kama icho. Akina Mo pamoja na utajiri wao lakini bado wanahustle. Aache uchovu na kulialia afanye kazi.

Akae akijua kuwa sisi sote anaotuona tunaishi tunapambana na mambo mengi hadi kuonekana hivi tulivyo. Fungate likiisha tunamsubiri stejini.
 
Wabongo mkiambiwa ukweli mnalalamika,mkidanganywa mnaona wivu na kuwaumbua wahusika. Vmoney kaamua kutoa la moyoni ili awe huru na maisha yake ya sasa.
Watu wote tunaishi kwa kuhustle. Chini ya mafanikio kuna vijimambo kibao vinavyowezesha mafanikio. Sasa hata ukisema ulie au ulalamike au utoe ya moyoni ukidhani labda ni wewe tu unayesota kumbe wote tunaokusikiliza tunasota na pengine kuliko wewe.
Asituone hivi, katika kumaintain hatua tulizofikia au kupiga hatua nyingine tunakutana na mambo mengi ya kuumiza.
 
Kila mtu ana namna ya kujipa nafuu mkuu hasa vmoney anayeogelea kwenye depression(mapenzi na music vyote vilimpiga vibaya)
Watu wote tunaishi kwa kuhustle. Chini ya mafanikio kuna vijimambo kibao vinavyowezesha mafanikio. Sasa hata ukisema ulie au ulalamike au utoe ya moyoni ukidhani labda ni wewe tu unayesota kumbe wote tunaokusikiliza tunasota na pengine kuliko wewe.
Asituone hivi, katika kumaintain hatua tulizofikia au kupiga hatua nyingine tunakutana na mambo mengi ya kuumiza.
 
Back
Top Bottom