NDUKI
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 3,423
- 2,414
Hilo fungu nadhani hukulielewa vizuri soma kwa makini.una maana mtu hapaswi kumwambia ndugu yake kuwa ulevi ni mbaya? maana katika fungu ulilosoma kuna sehemu pia inasema mtu asikuhukumu kwa vinywaji? Je unataka kusema Mtume Paulo alihalalisha kila anina ya kinywaji hapo? ndugu usikimbilie kukopi tu bila kuchunguza vizuri maana iliyokusudiwa katika fungu hilo.
Hilo fungu kwa ujumla linaongelea sherehe za kale za wana wa israeli ambao walilazimika kutoa kafara na sadaka za vyakula na vinywaji na kila baada ya mwandamo wa mwezi walifanya sherehe, kila baada ya miaka sita walifanya sikuu ya mwaka wa sabato ambapo hawakufanya kazi yeyote kipindi hicho. hayo mambo ndiyo Mtume Paulo alisema yaligongomelewa msalabani wala hatulazimiki kuyafuata kwa kuwa tunaokolowa kwa neema na hiyo neema ndiyo hutuongoza kuetnda mapenzi ya Mungu. Ndiyo maana sasa tunaomwamini Yesu Kristo hatutoi kafara ya wanyama, wala hatusherekei mwandamo wa mwezi wala hatuna sabato ya mwaka mzima kila baada ya miaka sita. Ila tuna amri kuu ambazo hazibadiriki kamwe na Mtume Yakobo anasema ukitunza zote ukajikwaa katika moja umevunja zote (yakobo 2:10).
Mkuu Ishmael umemuelewa vizuri Mkuu Kitaja...?.
Na je,umeielewa vizuri hiyo verse ya Colossians 2 : 16-17 mafundisho yake yazungumziwayo mkuu...?.
Last edited by a moderator: