Valentine na wizi wa maua ya makaburini...inasikitisha

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Iliwahi kuripotiwa mwaka jana...
Na mwaka huu imedhihirishwa wazi kuwa kuna baadhi ya watanzania washenzi wasiojua maana ya valentine na wasiojua mtakatifu Valentino alifanya nini mpk siku hii ikapewa heshima yake wameibuka na kubuni aina mpya ya Mradi.

Habari zilizothibitishwa kutoka kwa watu waishio karibu na makaburi zimesema kumekuwa na vitendo vya wizi wa maua yanayowekwa na wafiwa ktk makaburi ya wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.

Maua haya yanaaminika kupelekwa mkono kwa mkono kwa mahawala wa wezi hao, au pia maua haya hununuliwa bila kujua na malimbukeni wa siku hii ya Valentine.

Wizi huu wa maua ya makaburini umeshamiri kwa kiasi kikubwa miaka ya karibuni inapokaribia siku hii ya Valentine ktk mkoa huu wa Da'slaam, mkoa ambao unaaminika unaongoza Tanzania kwa kutukuza na kuabudu vitendo vya uasherati...
 
picture.php
Ntombo Lutete wa St. Eloi FC Lupopo akiipangua ngome ya Yanga
 
Back
Top Bottom