Kamati ya maadili ya Fifa imependekezwa Valcke apigwe marufuku miaka tisa
Katibu mkuu wa Shirikisho la soka duniani Fifa aliyekuwa amesimamishwa kazi Jerome Valcke ameondolewa rasmi kutoka kwenye wadhifa huo na shirikisho hilo.
Mfaransa huyo, 55, kwa sasa amesimamishwa kujihusisha na shughuli zozote za kandanda baada ya kudaiwa kuhusika katika njama ya kufaidi kutokana na mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia.
Fifa imependekeza apigwe marufuku kuhusika katika shughuli zozote za soka kwa miaka tisa.
Valcke, ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za ufisadi, amekanusha madai hayo.
Chanzo: BBC Swahili
Last edited by a moderator: