Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
STAA wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amefunguka kuwa kutokana na tumbua majipu ya Rais John Magufuli, wale mapedeshee waliokuwa wakiwategemea ni kama wamepeperuka kwani hawawapi fedha kama ilivyokuwa zamani.
Vai alifunguka hayo kutokana na madai kuwa, wasanii wengi wa kike wana hali mbaya na pale wanapopata mabwana wamekuwa wepesi kuchukulika hata kwa bei chee, tofauti na zamani.
“Kiukweli uongozi wa Rais Magufuli ni kiboko, hali ya maisha ni ngumu sana ndiyo maana hatuonekani kwenye kula bata kama zamani, nimeamua kufanya biashara zangu, filamu nazo hazilipi maana unaicheza kisha inakaa muda mrefu kabla ya kutoka, tumekomeshwa!” alisema Vai.