Ibrahimu hajawahi fika Makka
Alkaaba ndio nyumba ya Allah yaani ndio msikiti wenyewe; na ndio kiini cha ibada ya Waislamu ulimwenguni mwote. Nyumba hii ikidaiwa ilijengwa na Ibrahimu.
Muislamu yoyote asiposali kwa kuelekea kibra (ilipo alkaaba) ibada yake aiswii (kukubalika). Moja ya nguzo katika nguzo tano za uislamu ni kuhiji Maka kwa mtu mwenye uwezo. Hivyo ni tamanio la kila Muislamu duniani kufika hapo kabla hajafa. Wakiamini madhambi yako yote yanasamehewa ukifika hapo.
Ndio maana hata Mwijaku alifika hapo lakini mmmh. Hujaj yoyote yupo tayari kufia hapo kwenye alkaaba akiamini kama atakufa basi pepo ni yake. Hivyo wakifika hapo ni HARMAGEDON WAR ili kubusu jiwe jeusi iwe kwa amani au kwa show ya kibabe kama hiyo hapo unayoiona wakiminyana mbavu mbele za nyumba ya Allah.
View attachment 3326462
Uongo waliomezeshwa waislamu
Muislamu yoyote ameaminishwa kwamba alkaaba ilijengwa na Ibrahimu na mwanawe Ishamel. Hakuna uthibitisho wa kihistoria kwamba Ibrahimu alifika Maka zaidi ya ngano za Waarabu. Kutoka Canaan hadi Maka ni kilomita 1397. Hata Ishmael hajawahi ishi Maka, aliishi katika jangwa la Beersheba ambalo limeshikamana na jangwa la Paran.
Ndio maana alivyokufa Ibrahimu alikuja na kumzika pamoja na Isaka. Hivyo waliishi jirani tu. Sasa fikiria utoke Maka hadi Canaan kumzika mtu kwa usafiri wa Ngamia uweze? Hata kwa bus huwezi fika siku hiyo hiyo. Na kwanza atakuwa hajaoza tu? Au walikuwa na mochwari sio? Na nani alimpelekea Ishmael habari kwa umbali huo?
View attachment 3326466
Hivyo uongo wa Ibrahimu kujenga Alkaaba hauna tofauti na dai la Wakatoliki kwamba Petro ni papa wa kwanza na kwamba kanisa lililopo Vatican limejengwa juu yake. Alkaaba ilijengwa na waabudu miungu hasa mungu mkuu wa makabila ya mashariki aliyejulikana kama Baal au Hubali aliyeabudiwa na Waarabu na wakamwita Allah mungu wa mji wa Maka na Alkaaba.
View attachment 3326469
Na mjenzi mkuu wa ibada hiyo ni Wababeli na huko Hejaz aliyejenga ibada ya Hubali na mungu mwezi ni Nabonidas (mwabudu mwezi) mwana wa Nebukradreza.
View attachment 3326470
Na ndio maana hata leo mwezi na nyota ni ishara za uislamu maana eneo hilo kabla ya Uislamu waliishi waabudu mwezi.
View attachment 3326471
Ukweli sio rahisi kuzikwa.