Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti...

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,014
1,498
Umzaniae ndie kumbe siye, Ameumbika kwelikweli, mrefu wa wastani ana mwili mkubwa lakini sio tinginya,mweusi tii anameremeta akipaka mafuta, ana kifua kipana na manyonyo yaliyojazia, analo pia kalio linalotingishika akitembea. Niseme ule ukweli nilimtamani na baadae nikampenda kwa dhati.

Sikua na jinsi zaidi ya kujipendekeza, kwa haraka tukawa marafiki ila hakuwa tayari tuwe mwili mmoja, kwanini!?hakunambia na sikuweza kufikiri wala kuhisi kwamba anatat, nilidhani ni mbwembwe tu za usistaduu mpaka siku mmoja wa shoga zake alipotambua nyendo zangu kwamba namsarandia rafikie ndipo aliponitonya kwamba mwenzie anaugua.(ameathirika)ana ukimwi anatumia dozi kikamilifu. Sikuamini maskio yangu na bado siamini macho yangu, mdada alivyoumbika hakika kakamilika, iweje aishi na mdudu?

Bado najiuliza ila ndio hivyo tena "anao, anao, anao" Jamani nawasihi wanaume wenzangu tunapokwenda kwenye miji ya watu ama tunapokutana na watu tusiowajua na kuwahitaji kwa kufanya nao mapenzi tujipe muda kwanza ili kuwachunguza vinginevyo tuwe tayari kufa kimas'hara. (Muwe na usiku mwema wakuu)
 
We unaishi dunia gani mkuu?Anayetumia vidonge tena muda mrefu haambukizi cha muhimu tu usiwe mlafi ili umuandae muda mrefu ili uke utoe vilainishi.Pia unapiga sio kukomoana viwili vya afya au nazi mbili za mkwezi zinatosha kuepusha micchubuko mbona na mtoto mnazaa tena anakua hana maambukizi kabisa.
Umeboa ulivyosema anao anao kwani we bila maambukizi ndio utaishi miaka mia tatu kama kunguru?Au unafikiri utabakiaga peke yako wa mbegu???
 
Kwenye kampeni za CHAUMA takukuru wamezuia ubweche halafu we hata haujali! Ndo kwanza unaandika "uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti!" Kweli kila mtu na matatizo yake..
 
Tatizo liko wapi hapo?
Naona umemalizia andiko lako kwa unyanyapaa. Hivi wewe umepima hivi karibuni kujua hali yako kiafya?
Hivi ulimuuliza kuhusu hali yake kiafya?

Kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha na wala sio kigezo cha kuishi kwa shida, unyonge au kutokupendeza.

Kama wewe huna maambukizi ya VVU, na hutaki kuoa mwenye VVU, jua tu kuna wanaume wengi sana mwenye VVU wanaotafuta wenzi wenye VVU ili wajenge maisha pamoja.
 
kifo cha wengi harusi!!
Kwenye kampeni za CHAUMA takukuru wamezuia ubweche halafu we hata haujali! Ndo kwanza unaandika "uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti!" Kweli kila mtu na matatizo yake..
 
Umzaniae ndie kumbe Sie, Ameumbika kwelikweli, mrefu wa wastani ana mwili mkubwa lakini sio tinginya,mweusi tii anameremeta akipaka mafuta, ana kifua kipana na manyonyo yaliyojazia, analo pia kalio linalotingishika akitembea. Niseme ule ukweli nilimtamani na baadae nikampenda kwa dhati. Sikua na jinsi zaidi ya kujipendekeza, kwa haraka tukawa marafiki ila hakuwa tayari tuwe mwili mmoja, kwanini!?hakunambia na sikuweza kufikiri wala kuhisi kwamba anatatizo, nilidhani ni mbwembwe tu za usistaduu mpaka siku mmoja wa shoga zake alipotambua nyendo zangu kwamba namsarandia rafikie ndipo aliponitonya kwamba mwenzie anaugua.(ameathirika)ana ukimwi anatumia dozi kikamilifu. Sikuamini maskio yangu na bado siamini macho yangu, mdada alivyoumbika hakika kakamilika, iweje aishi na mdudu!? Bado najiuliza ila ndio hivyo tena "anao, anao,anao" Jamani nawasihi wanaume wenzangu tunapokwenda kwenye miji ya watu ama tunapokutana na watu tusiowajua na kuwahitaji kwa kufanya nao mapenzi tujipe muda kwanza ili kuwachunguza vinginevyo tuwe tayari kufa kimas'hara. (Muwe na usiku mwema wakuu)
Yalimkuta jamaa yangu jana baada ya kuwa na miadi na dada mkali sana for sure ni moja ya wanaweka unawafikilia katika akili yako.

But.......alifanikiwa kwenda na vipimo na kumkuta dada tayari anamaambukizi ya ukimwi nasema anamaambukizi .....

Tuache tabia ya kuangalia kwa macho na hii tabia ya kuangalia kwa macho imemfikisha jamaa yangu Engineer kupata maambukizi ya ukimwi kwa kujiridhisha kwa macho Eti mtoto hana hata kipele mean hana maambukizi.

Nasisistiza tuongeze umakini sana.

Sent from my SM-A605FN using JamiiForums mobile app
 
Kwaiyo nawewe uliishia kumskiza na kumuamini huyo shoga?

Je kama alikudanganya ili uwe nayeye?

na kama hupendi waathirika kwann msiende kupima ukapata huo uhakika ulioutaka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom