Uzuri wa magari ya automatic na manual...!!

He! Wanunulie manual wapate uzoefu.
Mimi watoto wangu wote nimewafundisha kuendesha manual. Hata wakinunua automatic lakini wanaweza kuendesha manual. Huwezi kuwa dreva mahiri kama huwezi kuendesha gari ya manual gear.
 
Ivi Manual zinatengenezwa tena kweli...maana nikiingia kwenye mtandao most of them ni AT....
 

Hapo utafanyaje sasa mdau GP maana ku-balance clutch na accelerator wakati mwingine kama kigongo ni kikali unaweza clutch inanuka (au akapita nyuki hujafunga dirisha akakudhuru unashangaa unaachia clutch), unapoweka hand brake sio unalizima linakuwa silence kama kawa ila lipo kwenye gia namba moja unakuwa umekanyaga clutch na brake ku-support maana handbrake inaweza fail sometimes (ila unashitua kiana kama hivyo una balance lakini kiaina). Hii naona ni nzuri kuliko hiyo ku-balance kwa sie wa kichina yaani handbrake ukitaka kuondoka unaachia huwa inabadilisha mlio wa injini ndio na wewe unatoa handbrake. kuzima halizimi labda uwe mwanafunzi kabisa hapo kasheshe maana mwanafunzi hata tambarare kuondoka linazima hata mara tatu.
 
Last edited by a moderator:
Ubadilishaji haraka wa Gia ambao unashangiliwa sana na wahuni vijiweni na vijana kwa ujumla yaani kabla mizunguko ya injini inayo hitajika kufika huua Gari. Hivyo kwa matumizi yetu injini ya AT itadumu zaidi ya ile ya Manual.
Jambo tu la kuongezea lakini naona arguments zilizo tangalia toka kwa wadau mbalimbali ni nzuri sana zinaongeza uelewa mkubwa.
 
Mkuu namimi nichangie kidogo. Mi naona kama kazi yako si udereva na upo bize sana na shughuli zako Automatic inakufaa kwasababu huitaji kutumia akili nyingi sana kuendesha, just weka D endesha, kuliko manual ambayo naona utahitaji akili ya ziada ya kubadilisha gia kila wakati. Lakini kama unahitaji kupata ladha ya kuendesha gari then manual ni safi. Otherwise mi naona zote ni sawa tu. MTAZAMO
 
Jambo wana jf
Mimi nina yote manual 4x4 na saloon auto.
Nafaidi manual ninapokua safari za mbali hasa rough road ila kwa mjin auto ndo ideal coz of folen.

Ukweli kwamba yote ni mazuri ila cha msingi ni matumizi ROI (return on investment) na unatumia ktk mazingira gani na kipato chako kikoje na pia hw competent ur r on the wheel?
Manual ni nzuri kwa mtu bahiri ila auto haikopesheki maana kama ni hydrolic imechoka...maana yake gia hazitaingia na itakulazmu ubadilishe. General service ya auto ni ghari compare to manual. Km betri imekufa manual unaweza kushtua, auto huwezi.
 

Kwenye fuel consumption nakukatalia, kwani AT ina program maalumu kwa ajili ya kupunguza matimizi ya mafuta na pia wear and tears. Manual zinagharama ndogo ukilinganisha na AT
 

We muongo. Enginw ya deseli ndiyo imara. Siyo Manual.
 
siyo kuwa discourage. Maana ya AT ni kuwa na vitu vingi mfano unakuwa na GPS ipo incorporated, n.k.
 
Naomba mjiulize. Je kuna gari lolote la Serikali ya JMTz au SMZ ambalo ni automatic? Je mnaweza tujuza ni kwa nini?

Sababu madereva na abiria wao(soma mabosi) ni BBC (Born Before Bomputers), kwao shida ina raha fulani hivi. kwa hiyo vile wanavyokukuruka na clutch, brake na accelorator, wanaskia raha fulani hivi....ndiyo sababu wanapendelea manual ukilinganisha na Auto.

Kwa sisi madereva wa hii digital age....tunapenda vitu soft touch...ni kwa mantiki hiyo Auto inanoga kuliko Manual.

By the way nadhani waliogundua Auto walikusudia kufanya driving iwe simple than it was before wakati wa akina volkswagen combi/beetle, peugeot 504, landrover 109, bedford, fiat mbaula, scania 111, leyland CD, Benzi mapua etc.
 
Asilimia karibu 80 ya magari yote madogo yanayotengenezwa sasa ni AT.

Kuna viwanda vya magari vimeacha kabisa kutengeneza manual, wao ni AT tu

Baada ya miaka kadhaa mbeleni magari yote madogo yatakuwa AT na manual itabaki hadithi tu

Dunia inasonga mbele na teknolojia inakuwa, manual inapitwa na wakati sasa.
Watu wanasumbua vichwa kurahisisha maisha na si kupigana kubadilisha gia,
Unaweka kitu kwenye D unaondoka na si mara klachi,mafuta na kuingiza gia kila mara
 

Source??...hapana mkuu,autos zimeanza kutengenezwa toka 80s huko,wangekuwa wana plan ya kuacha wangeacha long t..mimi nimejifunzia auto lakini saivi niko addicted na manual,huwezi kujiita dereva unless umeendesha manual..autos hata mwanangu wa miaka mitano Marcus naweza kumuelekeza akaendesha,you can't take any pride out of it..
 
kama sehemu unayoishi hakuna foleni na ni nje ya mji mkubwa hauitaji kusimama simama, nunua manual, lakini kama ni town, auto ndiyo mpango mzima.
 
siyo kuwa discourage. Maana ya AT ni kuwa na vitu vingi mfano unakuwa na GPS ipo incorporated, n.k.

hapa tunazungumzia automatic transmission bana, haihusiani na vikorombwezo vingine ambavyo hata kwenye gari ya manual vyaweza kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…