Uzuri na tabia huwezi kuvitenganisha ni kama kidole na kucha sana sana inategemea na mtu kipi anakipa uzito kati ya hivyo.
Uzuri na tabia huwezi kuvitenganisha ni kama kidole na kucha sana sana inategemea na mtu kipi anakipa uzito kati ya hivyo.
^^
Inawezekana kabisa! Jamii nyingi za zamani za Kiafrika walifanya jambo hilo kwa niaba ya vijana wao, na ndoa zilidumu.
Tofauti ya sasa na kale ni kuwa, kuna jambo fulani ambalo linakubalika katika ulimwengu wa roho lilifanyika ila sasa halifanyiki..yaani kuanza mahusiano na mtu mmoja na kuishi nae huyo huyo!
Ila uzao wa sasa, unakutana na mtu ana uzoefu wa kusifika zaidi ya wapenzi kumi, basi upatanisho unabaki mvuto tu
^^
katika kutafuta mwanamke mi ninaangalia zaid ananivutiaje,kwa sababu ukimchukua tu sijui unaingalia tabia inayorekebishika wakati wowote baadae unakutana na visura vya ajabu unaanza kutafuta mchepuko,na unakuta na tabia ulioingalia mwanzon na kubadilika ilishabadilika.mi naangalia uzuri bwana mengine hata kwa maombi yanabadilika,,
uko sawa kaisa mkuu,lakini wewe binafsi unaweza kutuambia ni nini unakipa uzito kati ya hivyo viwili?mke uliyenaye kwa sasa ikiwa umeoa ilikuwaje kuwaje mpaka ukaamua awe mwenzi wako?
nimekupata vilivyo mkuu,lakini nina maswali machache kwako,hapo kwenye red mkuu unafikiri ndoa zilidumu kwa ajili tu ya kuridhishwa na tabia za wenzi wao?au kwa kuwa tu kulikuwa na maadili ya hali ya juu hivi kwamba watoto wasingeweza hata kusema neno lolote la kuwakatalia wazazi wao?unaamini ndoa hizo zilidumu kwa ajili ya upendo uliokuwepo baina ya waliiooana au ni kwa kuwa watoto walikuwa tayari kufanya yote kwa ajili ya wazazi wao na maadili ya hali ya juu yaliyokuwepo kwa wakati huo?
^^
Macho yangu yameona mabinti wengi wazuri, wenye mivuto, maridadi, ni kama watakatifu walioshinda tuzo ya sayari ya Venus lakini tabia zao hata shetani anazivulia kofia
^^
katika kutafuta mwanamke mi ninaangalia zaid ananivutiaje,kwa sababu ukimchukua tu sijui unaingalia tabia inayorekebishika wakati wowote baadae unakutana na visura vya ajabu unaanza kutafuta mchepuko,na unakuta na tabia ulioingalia mwanzon na kubadilika ilishabadilika.mi naangalia uzuri bwana mengine hata kwa maombi yanabadilika,,
Mkuu mimi nilitumia kanuni ya neno la Mungu kuwa mwanamke mwenye busara/hekima/tabia njema mtu hupewa na Bwana,so cha kwanza ni tabia,nilifanya maombi ya kuatamamia nikiwa nimeambatanisha utashi wangu kwa Mungu...maana imenenwa haja zenu na zijulikane na Bwana,niliomba sana Mungu pamoja na tabia nilihitaji mwanamke mzuri kwa kweli.....maana imenenwa mtakula mema ya nchi hahaha.
Waswahili husema Mungu si ng`wana ong`wa kulwa nilikutana na huyo mke wangu ana sifa zaidi ya nilivyomuomba Mungu japo sikuwa namfahamu kabisa.Hivyo watu wasiogope kumuomba Mungu wakihofu kuwa watapewa wasiowataka.".........ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vilivyo vema si zaidi sana baba yenu aliye mbinguni..........."
^^
Ukimuuliza binti yeyote, ni taswira ya ipi ya mwanaume hataisahau, atasema ni yule aliyemtoa BIKRA,, hapa ndipo kuna maagano ya kiroho yaliyofanya ndoa nyingi zidumu. Pia upo ukweli usiosemwa, mwanaume pia humkumbuka mwanamke wake wa kwanza!
Kama mapatano hayo yalidumu, pia jamii ikaongeza sheria kali za kulinda ndoa basi mivuto lilikuwa jambo la mwisho kutazamwa, ila sasa ni la kwanza huku tabia ikiwa ya mwisho
^^
^^
Macho yangu yameona mabinti wengi wazuri, wenye mivuto, maridadi, ni kama watakatifu walioshinda tuzo ya sayari ya Venus lakini tabia zao hata shetani anazivulia kofia
^^
Tabia mwisho chalinze huku mjini ni urembo tu