Uzuri hupotea kama maua.

Uzuri hupotea kama maua.

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,657
Muda unakimbia. Maisha yetu hapa duniani yanaishia taratibu. Nashangaa nilikuwa mtoto sasa ni kijana. Natambua ujana huu ambao ni mzuri hautaendelea kukaa na mimi. Nina nguvu na sura nzuri lakini vitu vyote hivi vitapita. Wakati uzee utakapo nijia. Siwezi kuukimbia uzee utanichukua tu. Wakati huo miguu yangu haitofanya kazi vizuri. macho yangu hayataona. Mikono yangu ikitetemeka. Viungo vyote vya mwili wa binadamu vilivyokuwa vikifanya kazi havitafanya kazi tena katika nguvu ileile. Na simama na kufikiria ni nini maana ya maisha haya yanayopita kama upepo?

Natembea mitaani mjini posta naona wasichana wenye maumbo na sura nzuri. Kama maua uzuri wa mwanamke hautakaa milele ndani yake. Ni kitu kinachopita kama upepo. Utafika wakati wasichana vijana wote watakuwa wazee kitu kitachobaki ndani yao tu ni kumbukumbu ya uzuri waliokuwa nao.


Ujana ni mzuri lakini tuwe makini usitupoteze. Ukiutumia ujana vizuri uzee utaukumbuka kwa kumbukumbu ni za ujana.

Basi moyo wako usijawe na uovu. Jaza moyo wako kwa wema na uzuri wa mungu yeye apambaye maua na ndege wanaovutia. Kumbukeni maisha yanapita kwa kasi mno. Na huko tuendako hatukujui na wala tulikotoka hatu fahamu wote tumejikuta hapa duniani na tuwe na amani basi na tupendane.

Binadamu alipoumbwa na mungu alitafuta kiumbe kitakachoendana na mwanaume lakini alikosa miongoni mwa wanyama wote wa duniani. Ndipo mungu akampa usingizi mzito mwanadamu akamtoa ubavu wake na kumuumba mwanamke ili awe mwambata wake. Mtu ambaye atakaye ambatana nae na kuendana nae. Ndio maana katika dunia yote tuna watu wa aina mbili mwanamke na mwanaume. Watu hawa lazima waendane na wapendane na ni lazima kuwe na utaratibu ndio maana kukawa na ndoa sio tu kuparamiana kama mbuzi. Basi msichana atamuacha baba yake na mama yake na kumfuta mume wake hawa wawili watakuwa mwili mmoja. Ni lazima kuwe na muunganiko wa kihisia, kiakili, kiroho na kimwili. Love is more than lust. Love live longer, love endure and penetrate all things. But Lust destroy the hearts of men.
 
Awesome. I need more stuffs like this.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nakupa shavu la ukweli!mm penda vitu hivi ukweli mtupu na somo ni zuri!!
 
Nimependa sana maneno haya. Nadhani ntaprint ujumbe huu na kuuweka kumbukumbu.
 
nikfikria uzee natamani nibaki kwenye huu ujana lakini ndo hivyo sina hayo maamuzi.... Ubarikiwe kwa ujumbe mzuri
 
Be blessed! Umetukumbusha mambo muhimu coz tunajisahau sanaaaa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Haha hahaaa umeonaeeee... Watu wanataka mada za kugegedana tu lol wapi mzabzab kwi kwiiiiiiiii

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

hahaha wanawake wanaume wote twapenda kuongelea mambo ya kugegedana...asikudanganye mtu...binadamu twapenda dushelele na papuchi zinapoungana hahaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom