Uzuri hasa ni nini ?

Uzuri hasa ni nini ?

kitunguu saumu

New Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
4
Reaction score
8
Uziri ni kitu gani uzuri ? uzuri wapimwa vipi?
Uzuri upo dukani kama wanunua pipi?
Uzuri ule wa ndani , au umbo la halisi?
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri kalio kubwa linalozidi kiuno,
Kwenye nguo likakaba, likasheheni unono,
Akitembea si haba, wausikia mvumo,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri jicho jeupe, ukilona larembua,
Na tena wanja lipakwe, mizigo yote watua,
Ni kama lasema nipe, uende kulitungua,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Ama uzuri ni rangi, ile ya kimalikia?
Nyeusi na hudhurugi, ni zipi zakuvutia?
Lilo chaguo msingi, hata ndani kuingia,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri guu la bia, la kuvalia kimini,
Mwendo wa punda milia, unaotesa mjini,
Vile ulivyojazia, na hamasa ya chumbani,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri ama ni sura, wanaita mapokezi,
Kama mepimwa na rula, jinsi lilivyo amaiz,
Ikakukaa taswira hata kukaa huwezi,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri ama ni nywele zilojaa mabegani,
Zinawaka mwele mwele, kama wale walatini,
Sio mawigi ya mbali, yakutoa kabatini,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri kitu machine, isio mwaga mafuta,
Yani vyuma vinatane, bila boliti kuvuka,
Wastani iwe nene, harufu njema wapata,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri tabia njema, kwa wa nje na wandani?
Anapotaka kusema, anawaza kwa makini,
Anafanya yalomema, na kuyaweka manani,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri kushika dini, zile sheria za MUNGU,
Kwa kukesha ibadani, na sadaka za mafungu,
Kutubu madhabahuni, kwa machozi ya uchungu,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri ni hela nyingi, za kufanya matanuzi,
Ya ziada na msingi, bila kuwaza michuzi
Safari zilo kwa wingi, baada ya zako kazi?
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

Uzuri akili nyingi, yakuiseti mipango,
Yale mambo ya mzingi, ujinga kuweka kando,
Ushauri wake mwingi, kuunyoosha mkondo,
Uzuri hasa ni nini? Na upo sehemu gani ?

hakuna alokamali, kuyapata hayo yote,
weka tamaa za mwili, na akili usiache,
kupata mlo kamili, ni lazima ubalanse,
haya ni yangu mawazo, uzuri kwako ni nini ?
 
Kwangu mimi huyu ndio mzuri
Screenshot_20200423-152401.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa wenye sura za baba zetu tunasoma comments tuu
 
Back
Top Bottom