Uzoefu wangu kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye anajiweza kiuchumi

Niliwahi kuwa na mahusiano na mdada ana pesa zake za kutosha tu, yule dada alinizidi umri miaka 8 ila kwa miaka 2 niliyokua nae ktk mahusiano nili enjoy sana na nilikua huru sana. Alikua ananisikiliza kama mume, nilimshauri akanunua viwanja akafungua biashara zake (kabla ya hapo alikua anachezea tu pesa kwa kugawa kwa ndugu)...
Alikua akipanga twende tukale bata tunaenda kula bata hadi kuku wanaona wivu nilichokua nampendea pesa alikua ananipa nishike mimi kwahio ikija bill nalipa mimi (alikua anafanya hivyo ili nisijihisi mnyonge inferior) shopping pia ilikuwa hivyo hivyo pesa ananipa, nilikua muaminifu sana ikibaki Chenchi namrudishia japo alikua hatak mimi nilikua namuwekea ktk dressing table yake... Kwa wiki kunipa laki1 ilikua ni jambo la kawaida kwake... Kwa kuwa nae miaka 2 kiukweli alinibadirisha kimaisha na kifikra maana alikua na akili za maisha ila alikosa mtu wa kumpush azitumie vipi akil zake...
Ninachotaka kusema hapa wapo wanawake wachache sana, narudia tena wachache sana wenye akili kama za huyu dada... Wanawake wengi wakiwa na hela wanajiona wamemaliza maisha wanadharau waume zao mwisho wa siku wanaishia kuwa single maza na wanaishi kwa stress... Asikudanganye mtu wanawake wenye pesa na hawana waume wana stress kinoma wanajiona wanagundu...
 
Huo ujinga mwanamke hata anizidi kipato elimu cjui nini kwangu atabak kua mwanamke na akiniletea dharau na masimango najitoa cwezi kua mtumwa wa ngono na upare wangu ndo atanijua
 
Hili Taifa kama sio wazee wetu kujitoa tungekua Watumwa milele, yaan kijana wa aina yako ndio apewe jukum lakupiga na Mkoloni tungekomboka? Maana umeshindwa tu kujikomboa toka kwenye hiko kifungo cha mapenzi ukiwa na elimu yako haya wangekua wakoloni?
 
Sasa hapa si sawa na kununua malaya??? Tena bora ununue ujue mojaaa... Unatoa hela show unapewa ya kifalaaa
Screenshot_20220710-132335_Gallery.jpg
 
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuingia katika mahusiano na mwanamke ambaye alinizidi kipato.

Mdada alikuwa anafanya kazi katika idara fulani serikalini. mazingira ya kazi ya idara yake yalitengeneza mianya ya rushwa, hii ilimfanya awe anatengeza pesa nyingi za ziada nje ya mshahara. ifahamike hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa JK, mzee wa Msoga.

Mdada alijiimarisha sana kiuchumi kuanzia kumiliki majumba, magari na biashara mbalimbali.

Sikuwa vizuri kiuchumi wakati nikiwa nae kwenye mahusiano. there was a big financial gap between me and her. Hali hii ilinifanya niwe very loyal to her.

Girlfriend wangu alinizidi kipato licha ya kwamba nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani binafsi na kunifanya nisikose pesa mfukoni.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyojifunza katika aina hii ya mahusiano.

1: Mwanamke wa namna hii huwa very independent and confident. Hapendi umpangie ratiba zake wala kumuingilia kwenye mambo yake. Kama mmeenda kwenye starehe, muache ajiachie mpaka achoke, kwa mfano ukimzuia asiendelee kunywa bia ili mrudi mapema nyumbani atakasirika maana anajua anatumia pesa yake.

2: Kuwa mvumilivu pale anapopiga story na mashosti zake zinazohusu mikasa yao ya starehe au mahusiano na wanaume wengine. Usije ukaleta kiherehere cha kutaka kuhoji. Atakupiga biti.

3: Kubali kusimangwa, sina hakika kama wote wapo hivi, ila huyu wa kwangu alikuwa ananisimanga hasa akiwa amelewa. Kuna siku wakati tunarudi kutoka kwenye starehe nililazimika kushuka njiani baada ya kushindwa kuvumilia masimango ndani ya gari yake.

4: Jiamini, kuwa vizuri kimwili na kiakili. Mwanamke wa aina hii hapendi kudate na mwanaume legelege. Yaani uwe legelege kwenye kipato na kimwili?, hapana.
Vaa vizuri, nukia vizuri and don't forget to put your body in good shape by doing different exercises. wa kwangu alikuwa ananiambia kabisa nimekupenda kwasababu upo vizuri kimwili na kiakili. Possess knowledge about certain common things. Angalau uwe unajua baadhi ya vitu kuhusu computer au matumizi ya vifaa vya kidijitali. Be street-smart, usiwe mshamba mshamba.

5: Kubali kukatisha ratiba zako na kufuata ratiba zake. Usitoe excuse pale anapokupigia simu kukutaka umsindikize sehemu. Ukifanya hivyo atahisi unamdharau, jiandae kukaripiwa au kununiwa.

6: Kwenye mapenzi hakikisha unamridhisha yeye kwanza, yaani mpe dozi ya kibabe mpaka moyo wake uridhike na umfanyie vile vitu anavyopenda kufanyiwa kitandani. Usilete utundu wako wa kutaka kufanya vile vitu unavyovipenda wewe. Utamkwaza.

7: Usipende kuhoji mahusiano yake ya nyuma wala wewe usipende kusimulia mazuri ya EX wako. Atakwazika.

8: Usimpangie matumizi hata kama unahisi fedha anazotumia zinazidi kiwango. Muache atumie vile anavyotaka. Kumbuka ni zake.

9: Sifia umbile lake au mavazi yake hata kama unahisi siku hiyo hakupendeza.

10: Mzawadie zawadi hata kama ina gharama ndogo. ataipokea na ataithamini.

11 :play your part by becoming her comforter during her difficult times. Kuna wakati anaweza kukuelezea changamoto mbalimbali za kazini kwake, biashara zake, ndugu zake au marafiki zake. Usiwe sehemu ya kuzidisha tatizo. Wakati wa mazungumzo msikilize na mwisho uje na masuluhisho sahihi.

Hayo yote hayana shida kama una malengo yako.

Kiufupi hautampenda maana ile hali ya mwanaume kuwa mwanaume inakuwa haipo tena. Ila utakuwa umependa pesa zake na kikubwa ni uzipate hizo pesa ufanye mambo yako.

Kwa jinsi ulivyoandika ni kwamba hamko pamoja tena (jambo ambalo halishangazi).

Ila nina shauku ya kujua ilikuwaje mkaachana, na je ni wewe uliyemuacha au ni yeye aliyekupiga chini akahamia kwa kidume kingine?

Kama ni yeye aliyekuacha je aliamua kuambatana na mwanaume mwenye sifa gani? Yaani huyo mwanaume wake mpya na wewe jamaa kakuzidi nini?

Halafu pili, ukiwa kama mwanaume, ni lazima ulikuwa unahitaji mwanamke ambaye unammiliki. Je uliweza kufanya hayo ukiwa na huyo Boss Lady, au alikuwa anakubana kisawasawa?

Na je pesa zake huyo Boss Lady ulizipata, na ulikuwa unazipata kwa staili ipi?
 
We ulikuwa mnyonge tuu ...huwezi kuwa royal namna hiyo hata kama huna hela
neno sahihi ni "loyal" na sio royal(kwa maana ya muktadha wa kile nilichoandika kwenye uzi wangu).

hata hivyo nimekulewa ndg.
 
Hayo yote hayana shida kama una malengo yako.

Kiufupi hautampenda maana ile hali ya mwanaume kuwa mwanaume inakuwa haipo tena. Ila utakuwa umependa pesa zake na kikubwa ni uzipate hizo pesa ufanye mambo yako.

Kwa jinsi ulivyoandika ni kwamba hamko pamoja tena (jambo ambalo halishangazi).

Ila nina shauku ya kujua ilikuwaje mkaachana, na je ni wewe uliyemuacha au ni yeye aliyekupiga chini akahamia kwa kidume kingine?

Kama ni yeye aliyekuacha je aliamua kuambatana na mwanaume mwenye sifa gani? Yaani huyo mwanaume wake mpya na wewe jamaa kakuzidi nini?

Halafu pili, ukiwa kama mwanaume, ni lazima ulikuwa unahitaji mwanamke ambaye unammiliki. Je uliweza kufanya hayo ukiwa na huyo Boss Lady, au alikuwa anakubana kisawasawa?

Na je pesa zake huyo Boss Lady ulizipata, na ulikuwa unazipata kwa staili ipi?

kama umesoma vizuri uzi wangu,kuna sehemu nimendika kwamba nilidate na huyu mwanamke kipindi cha utawala wa JK.

ni miaka kadhaa sasa sipo ktk mahusiano ya kimapenzi na yeye.

last month alinipigia, lengo hasa lilikuwa ni kuniomba nimuazime laki tano ili a sort out issue ya ada ya mtoto wake. mpaka hapo unaweza ukang'amua kwa sasa yupo ktk hali gani kiuchumi.

una swali lingine ndg?.
 
kama umesoma vizuri uzi wangu,kuna sehemu nimendika kwamba nilidate na huyu mwanamke kipindi cha utawala wa JK.

ni miaka kadhaa sasa sipo ktk mahusiano ya kimapenzi na yeye.

last month alinipigia, lengo hasa lilikuwa ni kuniomba nimuazime laki tano ili a sort out issue ya ada ya mtoto wake. mpaka hapo unaweza ukang'amua kwa sasa yupo ktk hali gani kiuchumi.

una swali lingine ndg?.
Maswali niliyouliza hujayajibu. Naomba uyajibu moja moja.
 
Back
Top Bottom