illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
nilifungua akaunti ya mshahara katika benki tajwa miaka kadhaa iliyopita, mara kwa mara afisa mkopo akawa ananishawishi kuchukua mkopo, baada ya kuona kweli nija uhitaji wa mkopo ikabidi nianze kufanya tafiti katika benki mbalimbali ili nione ipi yenye ahueni...kwa kua kwa sasa technologia imekuwa nika tembelea tovuti mbali mbali za benki tofauti, nilipoangalia kwenye tovuti ya benki tajwa nikavutiwa kwani inaonyesha wanatoa mkopo mara ishitini na tatu ya mshahara wako, basi siku inayofuata nikaenda mpaka kwa yule afisa mkopo lakini akaniambia hawatoi kiwango hicho na kuniuliza nimetoa wapi hizo taarifa.
Kwenye tovuti yenu sikutaka kubishana naye nikamwomba anikokotolee kiwango nachoweza kupata kulingana na mshahara wangu ambapo aliniambia ni milioni 14 basi akanichapia karatasi lililoainishwa kila kitu ikiwa ni kiwango cha mkopo, muda wa makato, kiwango cha riba (22%) nikampelekea mwajiri wangu nikawa nasubiri hela iingie, nikasubiri baada ya muda nikapigiwa simu kuwa kuna karatasi natakiwa nisaini ili kesho yake niweze kupata hela basi nikaelekea tawini nikafika nikakuta karatasi tofauti na lile la awali lenye makokotoleo hili linaonyesha kuwa riba ni asilimia 24.9 na kwamba ntapata m 12.8 pekee nikauliza kulikoni wakanipa majibu ya kihasibu ambayo hata sikuyaelewa nikawambia kwa riba hiyo siko tayari wakasema haiwezekani kwa kuwa wameshafanya taratibu zote mpaka hela imeshawekwa bado ku akisi ( reflect) tu kwenye akaunti yangu na mimi nikafikiria kwa sababu nakala pia nishampelekea mwajiri siwezi kufuta utaratibu wote.
Kwahiyo ule mkataba wa mwanzo wenye riba asilimia 22 tukauchana nikatia sahihi kwenye huu mkataba mpya. na kweli baada ya masaa kadhaa wakaniwekea hizi m 12.8 .....ikabidi nimpelekee mwajiri mkataba mpya na kumwambia ule wa awali hautatumika tena ambapo nilikuwa na wakati mgumu kumuelewesha mpaka akaniamini..swali ombi ama pendekezo kwa faida ya wateja wenu kwanini msiweke wazi riba na gharama zingine zozote badala yake haya mambo yanafanyika kijanja janja....waambieni wateja kabisa kuwa riba yetu ni hii na kwa mshahara wako utapata kiasi hiki utakatwa kwa muda fulani ili mtu akiamua awe anajua anachokifanya kuliko kumbadilishia mtu mkataba dakika za mwisho na sisi wengine sio wahasibu.
Natafuta hela nilipe deni lote niachane na nyinyi kabisa