Uzinzi ni uzoefu mbaya kwenye ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinzi ni uzoefu mbaya kwenye ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jayfour_King, Jan 2, 2010.

 1. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifikiri sana jinsi ambavyo ndoa tulizo nazo siku hizi zilivyo na matatizo lukuki. Ingawa ndoa na sherehe zake siku hizi ni aghali sana ukilinganisha na za zamani lakini bado hazina thamani wala guarantee zaweza vunjika wakati wowote.

  Nimejaribu kufuatilia na kuona kwamba sehemu ya matatizo hayo hutokana na sababu zifuatazo:
  Zamani ilikuwa ni aibu msichana kukutwa hana bikira siku ya ndoa yake. Kwa baadhi ya tamaduni hili likidhihirika (hana bikira) ndoa yaweza kuishia hapo na msichana kurudishwa kwa wazazi wake labda kama itathibitishwa bila kivuli cha mashaka kwamba sababu za kukosekana bikira hiyo ni sababu za kimatibabu, vinginevyo sherehe zinaishia hapo kwa maelezo kwamba ndoa haijajibu.

  Hivyo wasichana wa wakati huo walikuwa wanajitunza kuepusha aibu ambayo yaweza kuja kumkuta siku yake ya ndoa yeye na wazazi wake. Kwani kwa mila za wakati huo suala la msichana kuwa bikira ndilo linalotegemewa na jamii nzima na halikuwa na mjadala. Na ikitokea vinginevyo kijiji kizima kitafahamishwa kuhusu kituko hicho. Tofauti na sasa ambapo msichana kuwa na bikira anajiona kama mshamba vile!

  Tatizo la kuiga utamaduni wa kizungu (girl friend and boyfriend) ndio kwa maoni yangu unaofanya ndoa nyingi zishindwe kusimama imara. Uhusiano wa namna hii huleta matatizo kwenye mahusiano ya baadaye ya ndoa kwa sababu, fikiria kwamba huyu boyfriend au girlfriend uliyenaye sasa siye utakaye funga ndoa naye.

  Madhara yatakayo jitokeza hapo ni kwamba, pamoja na kwamba tunaamini binadamu wote ni sawa ni kwa mahitaji muhimu tu, lakini tunatofautiana kwa maumbile, matumizi ya maumbile hayo, mitindo na mambo mengine. Tatizo kwenye ndoa huja pale ambapo msichana kwa mfano, boyfriend wake wa mwanzo aliyelianzisha alikuwa na big pipe halafu akaja kuolewa na bwana ambaye sehemu zake ni kama kidole cha mkono hivi! Kwa mazoea ya mwanzo tayari hili linaweza lika lead kwenye mis-satisfactions na hivyo inaleta ulinganisho wa between two, who is the best. Hivyo kama yule boyfriend wa mwanzo bado yupo yupo anaweza kujishindia tenda ya wizi.

  Au kwa mfano msichana uliye kuwa naye kama girlfriend wako alikuwa na maumbile madogo na hivyo ulimzoea na kumpenda hivyo halafu mamsapu anakuja kuwa na kisima fulani vile na maji hayakauki (mdebwedo) hii tayari itakufikirisha kuona kama vile umekosea, au umeuziwa mbuzi kwenye gunia !

  Hitimisho: Kwa maelezo hayo utaona kwamba matatizo yanatokea kwenye ndoa kwa sababu mnaingia kwenye game kila mmoja ana uzoefu wa kwake na ni tofauti. Na haiwezekani tofauti ya uzoefu huu ukawaridhisha wote. Ni lazima atakuwepo gainer na looser, kwa hiyo looser ni lazima ata keep on searching.

  Wakati ambapo ilitakiwa muanze wote mkiwa hamjui upi ni mtarimbo doro, kisima maji mengi, wala kuchelewa kufika mlimani! Na yote hayo mnatakiwa kujifunza mkiwa pamoja ili mvivu mazoezini aongezewe mazoezi ndivyo mambo yanavyopaswa kwenda.
   
Loading...