Uzinzi, dhambi namba moja duniani

Nipe Andiko

Senior Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
133
Reaction score
133
Nionavyo mimi, kuzini ndio dhambi ambayo inaangusha wengi kuliko zote. Watu wengi wanaamini kwamba hawawezi kukaa bila kufanya ngono hadi siku watakapooa rasmi.
Wanaona kuwa kukaa bila kufanya mapenzi ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Hivyo basi wengi wameamua kufanya uasherati na uzinzi kwa sana, kwa sababu wanafikri ni jambo lisilokwepeka.

Imefikia hatua kwenye jamii zetu, mtu akionekana hajihusishi sana na mambo ya mapenzi, hasa wanaume, basi anatiliwa mashaka na kuonekana kwamba pengine hayuko sawa kimaumbile, mfano labda jogoo hawiki n.k

Na wale ambao ni play boys, ambao hawapitwi mbele na sketi, eti hao siku hizi ndio wanaonekana, majembe, wanaume wa ukweli, tofauti na wale ambao hawajishughulishi na ngono ambao huambulia kejeli na matusi kibao.

Sasa sijui tumerogwa na nani?
Yaani uzinzi umekuwa fasheni, ukiufanya unasifiwa, ukitulia usifanye ngono ovyo, unatukanwa. Na kuitwa majina ya ajabu ajabu.

Leo hii, mawazo karibia ya vijana wote ni uzinzi mtupu, wanawaza ngono tu, kama huamini, fanya research hata kwenye mitandao ya kijamii, utaona uzinzi ulivyoota mizizi, nenda kwenye groups za WhatsApp uone jinsi vijana wanavyoshinda wakitongozana tangu asubuhi mpaka usiku wa manane, nenda fb, nenda Hitwe, njoo jf, n.k Kutongozana kunaenda sambasamba au hata kuzidi mada zingine zote mitandaoni.
Wnafunzi wanaoenda vyuoni pia kando na kusoma lengo lingine ni kwenda kuendekeza uzinzi chuo.

Kijana akiona binti, wazo la kwanza linalomjia kichwani ni kufanya naye mapenzi, atajitahidi mpaka alale naye. Ndio maana hakuna urafiki wa kudumu kati ya binti na kijana.

Watu wazima, wasomi na akili zao, wameacha wake zao nyumbani, wamehamia kwa michepuko.

Iwe shuleni, kazini, nyumbani, Kanisani, Msikitini, Chuoni, KOTE HUKO. NGONO NDIO HABARI YA MJINI.

Matokeo yake ni ndoa kuvunjika, magonjwa, kifo na mwisho KUKOSA UZIMA WA MILELE.

KUACHA UZINZI INAWEZEKANA, AMUA UTASHINDA! MUNGU HAKUTUPATIA AMRI NZITO TUSIYOWEZA KUISHIKA, AMRI ZOTE NI NYEPESI NA ZINASHIKIKA.

Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

1 Yohana 5:3
 
Wamebarikiwa wale ambao katika Zinaa Ni wajiepushao
 
Nimekupata vema mkuu ila nasikia maandiko yanasema hakuna dhambi ndogo wala kubwa.Zote ni sawa kabisa
 
huu ni mtihani ni Mungu tu wakutuokoa Gal5:16- 22 basi enendeni kwa Roho kamwe hamutatimiza tamaa za mwili....
 
Unaweza kujizuia kuiba, unaweza kujizuia kutokudanganya, unaweza kujizuia kuacha ulevi bangi, pombe na vinginevyo lakini kugegeda hakuna aliyemkamirifu anayeweza kujizuia
 
Pia watu wanasahau sana kwamba "Yesu ni Yesu hata kama baba yako fundi seremala" Mungu yupo tupunguze makinikia
 
Baba mchungaji tuma copy ya huu ujumbe wako pale magogoni kuna mpangaji wetu pale nasikia huu mtihani umemshinda kabisa
 
Baba mchungaji tuma copy ya huu ujumbe wako pale magogoni kuna mpangaji wetu pale nasikia huu mtihani umemshinda kabisa
Duuu[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Kuanguka ni matokeo ya kujiingiza kwenye tamaa za mwili kufanya zinaa na watu tofauti tofauti inayo pelekea kupoteza kinga za kiroho na nguvu za kimungu ndani ya MTU
 
Hakuna Dhambi ndogo wala kubwa ila Dhambi ya zinaa imetofautishwa kabisa na dhambi zingine zote

Biblia inasema dhambi nyingine zote zafanyika nje ya mwili huu ila zinaa inafanyika ndani ya mwili

PIA zinaa ni dhambi inayoambatana na LAANA na MAROHO YA AJABU endapo utazini labda na nduguyo au mtu yeyote mwenye asili ya ushirikina na roho chafu

Ukizini na mtu wa namna hiyo ni wazi utabeba mambo yake yooote

Kingine ni kwmba dhambi ya uzinzi inamfanya Mungu awe mbali na mtu hivyo itazuia baraka zako na kukufunga na pia dhambi ya Uzinzi au uasherati ingawa inafanyika kwa siri ila itakuletea AIBU mbele za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…