Uzinduzi wa Usafirishaji mizigo kwa SGR

Uzinduzi wa Usafirishaji mizigo kwa SGR

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Uzinduzi Treni za Mizigo SGR.jpg
sg
 
Kiti cha mbele kabisa...A new Era in Tanzania 🙏
 
Kwanini hamfanyi maboresho yoyote kwa Dar es salaam commuter train?
Abiria ni wengi sana, lakini nyinyi mnapunguza behewa kilakukicha na hamfuati ratiba.
Suburban rail ya Ubungo ni kama imeshakufa, kutoka behewa 10 mwaka 2012 ilipoanzishwa mmebakiza behewa tatu huu mwaka 2025.
Suburban rail ya Pugu mmepunguza behewa toka behewa 20 mwaka 2012 mmebakiza behewa 10 mwaka 2025

Kushindilia abiria kama vifurushi kuna hasara nyingi:
Kupoteza mapato maana kuna watu watapanda bure kutokana na kujazana sana.
Kuambukizana magonjwa sababu ya kukosa hewa.
Kupoteza muda wakati kushusha au kupakia vituoni, abiria anatumia muda mwingi kutafuta upenyo wa kupita ili ashuke au apande.

Suburban rail zote, Ubungo na Pugu hamjaweka miundombinu ya kuwezesha mtu mwenye ulemavu kuweza kutumia huduma ya train, abiria mlemavu hawezi kuingia kwenye train hadi abebwe na watu kuingizwa ndani.
Kwa muundo wa ngazi za behewa zenu, siyo tu mlemavu bali hata abiria mzee, hawezi kukwea zile ngazi

Commuter train ni huduma bora sana endapo itafanyiwa maboresho, na kuondoa kero zinazokwaza abiria.
Behewa zinapunguzwa siyo kwasababu hakuna abiria, hapana! abiria ni wengi sana, hadi wengine hukosa nafasi hasa train ya saa 12 jioni. Mnapunguza behewa sababu ya ukosa ubunifu na management isiyo imara!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom