Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Serikali imekusanyika Tanganyika Packers, Kawe kuzindua Kanisa la Arise & Shine la Boniface Mwamposa. Televisheni ya Taifa ipo mubashara (LIVE).
Tanganyika Packers LTD, Kawe, Dar es Salaam 1945-1975. Kilikuwa kiwanda cha kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.
Eneo la Mloganzila (Muhimbili) lilikuwa ni eneo la Tanganyika Packers LTD na ndilo eneo lililokuwa linatumika kuwapokea na kunenepeshea ng’ombe.
Walipoletwa kutoka mikoani kwa treni waliteremshwa katika Stesheni Pugu, baada ya mwezi wanaswagwa kupelekwa Kawe kuchinjwa na kuchakatwa.
Kutoka Mloganzila hadi kiwandani (Kawe) wakati wa kuswagwa, waingereza waliita COWS WAY (njia ya ng’ombe). Waswahili wao wakaamua kuita “KAWE”
Tanganyika Packers (TPL) kilikuwa kiwanda kikubwa, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje mpaka kwa malkia wa Uingereza,
Kilikuwa kiwanda tanzu cha shirika la LEMCO (Liebig’s Extract of Meat Corporation) linalofadhiliwa na Uingereza, na lilianzia miaka ya 1860 Uruguay.
Liebig ni heshima ya baba wa (Organic Chemistry), Justus von Liebig. Jengo la machinjio la LEMCO linapatikana katika Urithi wa Dunia wa UNESCO.
Sehemu kubwa ya nyama kutoka Tanganyika Packers iliuzwa Ulaya hususani katika nchi ya Uingereza. Watanganyika walipata ajira katika kiwanda.
Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa na wakoloni kutoka Uingereza 1945 na kilitoa zaidi ya ajira 2,500 ambapo 1,200 zilikuwa ni ajira za kudumu.
Walifanya kazi kwa kupokezana (shift), walichukuliwa kwa mabasi hadi kazini. 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kufuatia sera za ujamaa.
Kiwanda kilizalisha nyama za mabuchani, mafuta ya kutengeneza sabuni, damu ya ng’ombe ilikaushwa na mifupa ilisagwa na kuwa chakula cha kuku.
Pembe na kwato za ng’ombe zilichemshwa kwenye boiler zikatoa gundi, kiwanda pia kilisindika nyama na maharage kama ox-tail beans, ngozi etc.
Katika vita ya Kagera 1978-1979, kiwanda kilitumika kuwalisha wapiganaji vitani. Chakula cha kusindika kilitoka kiwandani kwenda uwanja wa vita.
Mwaka 1975 Serikali ya Mwl, Julius Kambarage Nyerere ilitaifisha kiwanda cha Tanganyika Packers na kukifanya kuwa mali halali ya Serikali ya Tanzania.
Baada ya Serikaki kutaifisha kiwanda, uzalishaji na ubora wa nyama iliyosindikwa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kukosa utaalam na ufundi endelevu.
Serikali walinyimwa leseni ya kusafirisha nyama iliyosindikwa. Walinyimwa (phytosanitary certificate) kuthibitisha ubora wa vyakula vya kusindika..
Waingereza wakawanyima cheti cha ubora na usafi wa nyama inayozalishwa. Soko la Ulaya ambako ndiyo walikuwa wanunuzi wakubwa, soko likapotea.
Soko la ndani likawa gumu kiwanda kikaanza kusambaza nyama zake kwenye mabucha ya ndani ya Dar es Salaam na mwaka 1992 kiwanda kikafariki.
Taratibu kiwanda cha Tanganyika Packers kikaanza kufariki vibaya sana. Baadaye kilibinafsishwa kwa mbunge wa Kawe, akauza mashine na vipuri.
Mbunge wa Jimbo la Kawe wakati huo, Zainuddin Adamjee (CCM), aliposhindwa kukiendeleza kiwanda hicho akaamua kung’oa mitambo na vipuri. Akauza.
Mapaa, madirisha, milango na vifungashio vilipelekwa Mapambano (veterinary) na kupimwa vyuma chakavu (scrappers) na mapaa yaliuzwa kama vifaa used.
Picha hiyo chini, inaonesha ng’ombe wakiwa Tanganyika Packers kabla kiwanda hicho hakijataifishwa. Sehemu ambayo pamepewa jina jipya - nyumba ya upako
Soma Pia: Rais Samia akishiriki Uzinduzi wa Hema la Mwamposa, Julai 5, 2025 Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe
Leo Tanganyika Packers palipokuwa KIWANDA kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa KANISA. Watu watauziwa udongo na mafuta na maji. UPAKO.
Leo Tanganyika Packers watu ndiyo kondoo na wanajipekeka wenyewe machinjioni. Wananyweshwa maji na kulishwa udongo wakielezwa ni UPAKO.
Kanisa la MWAMPOSA (wao wanamuita MTUME) linawaombea maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira ili wapate ajira kwa maombi.
Leo ingelikuwa hilo ni kusanyiko la kuzindua kiwanda cha kusindika na kusafirisha nje ya nchi nyama na mazao ya mifugo, hakika, ningemwaga pongezi nyingi.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.