Uzinduzi wa Kampuni ya simu ya HALOTEL Live TBC

Uzinduzi wa Kampuni ya simu ya HALOTEL Live TBC

Dah niliwasubir kwa hamu kubwa kweli inabidi niendelee kuyakubali maisha ya tigo
 
Watakuja kukaa vizuri tu kwani mipango yao ni madhubuti...wanafanana na waliopo wakati wao ndio wanaanza...hakika wataleta upinzani...hasa sehemu zisizokuwa za mjini..
 
kampuni ya kivietnam hiyo ina wanyanyasa sana wafanyakazi wao unafanyishwa kazi kama mwana jeshi, kilakukicha watu wanaachishwa kazi
faida ya uwekezaji huo ni nini

Wanabebwa sana na serikali kwakupewa maeneo ya serikali bure kuweka mnara wao au kwakukodi maeneo ya wa nchi kwa bai ya chini sana.
 
Hahaha wabongo bwana, kutwa kucha kulalamika. Kazi zilikuwa tatizo wakawa wanalalamika, amekuja mvietnam na pesa zake kutoka kwake na kila kitu chake, kaleta ajira kibao bado wanalalamika. Technology inayotumika ni ya quality kubwa kuliko mitandao mingine na uwekezaji wake ni gharama zaidi ya lakini mimi kama mtanzania nataka huduma nipewe kwa bei rahisi zaidi. Hiyo mitandao mingine ina zaidi ya miaka kumi nchini hapa lakini kuna sehemu kibao network hakuna kabisa na hata maeneo ya mijini kabisa unakuta network ni ya kupandia milimani, lakini huyu mpya kwa muda wa chini zaidi ya mwaka mmoja ameweza ku-cover eneo kubwa zaidi ya hawa wakongwe na tena wakongwe haswa. Makao makuu ya mikoa tu kwa mitandao mingine 3g imekuja hata mwaka mmoja na nusu haujafika lakini huyu anapeleka 3g kila makao makuu ya wilaya. Jamani hata kama mnakuwa wapinzani jifinzeni kupinga kwa hoja zenye mashiko. Yeyote ambaye ameshafanya calls za halotel kwenda Halotel aje aseme call quality ikoje.
 
Wote wanyonyaji tu!wafunge safari ndefu kutoka vietnam mpaka bongo waje wakupe huduma tu....!
 
Mnaangaika na kutafuta kubadirisha line kwa ujio mpya, kila siku nawapa habari za hawa #ZANTEL mbona wana huduma na viwango vya chini kuliko kampuni yoyote au hata hiyo halotel?

Kuna kampuni gani ya simu kwa shs 300 wanakupa 7mins, 100sms mitandao yote na 25mb..?
 
Hiyo no Vietel kampuni ya jeshi la wavietnam.

Hawa hawajaendelea kwao kama sisi ni umburula tu unaotufanya tuamini kuwa ni wawekezaji wa maana!! Hawana jipya ni muendelezo ule ule wa 10% za kuhonga wakati wa uchaguzi unaofanywa na hawa magamba!! Wanaharibu mandhari ya miji yetu kwa tekinolojia ya zamani kwa kuweka minara kila mahala inayohatarisha afya za wananchi!!
 
Mnaangaika na kutafuta kubadirisha line kwa ujio mpya, kila siku nawapa habari za hawa #ZANTEL mbona wana huduma na viwango vya chini kuliko kampuni yoyote au hata hiyo halotel?

Kuna kampuni gani ya simu kwa shs 300 wanakupa 7mins, 100sms mitandao yote na 25mb..?

Tatizo upatikanaji wa credit zake ni mgumu mno
 
Tatizo watanzania tunapenda starehe kuliko kazi. Wenzetu wanaendelea kwasababu wanawekeza katika kazi. Lakini sisi tunataka kazi ndogo tulipwe milioni. Hawa jamaa niliwaona sehemu wanapandisha mnara, wale jamaa huwa wanalala hapo hapo hata kama ni kichakani. Wanawekeza katika kazi na si kama sisi muda wote tunalalamika, mfanyakazi wa serikali anakuja anapiga stori mpaka saa9 anarudi nyumbani halafu mwisho wa mwezi anakula pesa ya kutosha na mwisho anaona anastahili pesa ile kwa kazi hiyo aliyoifanya na mwisho anageuza hicho kuwa kipimo cha utendaji kazi in relation na malipo unayostahili. Tutachukua muda mrefu sana kukaa katika senses na kujua nini kiwe kipaumbele.
 
Hawa wangeenda nchi zisizo na mawasiliano huku Tigo, Voda, Airtel tayari wameshika soko
 
Siku zote nilikuwa naona gharama za mawasiliano tz zipo juu sana..lkn nimetoka kidogo nje ya nchi moja jirani..gharama zipo juu sana..sh 2000 ya tz unapata mb 80. Kwa siku.sh 1000 ya tz unapata mb 30.wkt kwa bongo sh 1000 unapata mb 800.hiyo si nafuu mara ngapi?
 
Back
Top Bottom